JAMANI NISHAURINI JUU YA HUYU MUME WA MTU....
Written by Mange   
Monday, 15 March 2010 19:26

Hi Mange

mi nilikuwa naomba ushauri juu ya huyu mume wa mtu.Huyu mkaka ni kwamba alikuwa anaishi na mkewe huko Mwanza sasa akahama kikazi akaja hapa Dar akamwacha mkewe huko Mwanza anaendela na kazi alipofikisha karibia miezi sita akamwambia mkewe aje kuishi nae hapa mkewe akakataa kabisa sasa yule kaka akaendelea kuishi hapa akawa anaenda au mkewe anakuja wakti wa likizo kumbuka hapo wana mtoto mmoja tu.Sasa huku kazini nikawa nimekutana nae mie na kwa mara ya kwanza sikujua kama ameoa kabisa ila baadae aliniambia na akasema ananipenda sana basi tumeendelea na uhusiano mpaka hivi sasa. Ila sasa yule mkewe kumbe akawa kuna mtu anatoka nae kule Mwanza na mapenzi mazito kiasi kwamba kila mtu mpaka ndugu wa mwanaume wakajua na wakamshauri aachane nae maana anatia aibu sana huko Mwanza basi mkaka akaona hapa ndiyo safi akaniambia kuwa anataka kunioa mie na yuko serious mpaka kaanza kunitambulisha kwa ndugu zake na mkewe kashamwambia hataki.

Sasa nie sijajielewa nikubali hii ndoa au nikatae maana naona inanichanganya sana.

Naomba ushauri kwenye hili na kumbuka mwanaume nampenda pia

Mdau,Martina


Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Comments
Add New Search
Anonymous   |2010-03-15 16:11:16
wewe nimshenzi sijawahi changia humu lakini imebidi nichangie umeniudhi sana
ungekua karibu yangu ningekuslap.ndio nyienyie tunawatafuta husband snacha mimi
ni binti tu sijaolewa lakini nachukia sana mwanamke anaye tembea na mume wa
mwenzanke tena akitambua kabisa ni mume wa mtu.wewe umejua huyo ni mume wa mtu
umetoka naye wanini.? hata kama mkewe anatembea na mtu mwingine wewe inakuhusu
nini?na wewe unajuaje ni kweli au ni manenotu yawatu wewe umeshawahi mshika mguu
huyo mwanamke ?
nakwambia the samesame unavyo mfanyia mwanamke mwenzako
kwakumtembelea na bwana ake ndio hivyohivyo utafanyiwa malipo ni hapahapa
duniani.alafu bila aibu kabisa eti unataka kuolewa unaolewa kwenye ndoa ya
mwenzako alafu unategemea utaishi kwaamani unajidanganya hutopata amani
hatasikumoja.umenikera sana malaya wewe Tafuta mumeo mshenzi wewe ukikosa baki
nunga embe lol wanawake tuna roho mbaya muhurumie mwanamke mwenzako na mtoto
lol.shame on ur...
Anonymous   |2010-03-15 20:51:51
Ha ha haa!
mwanamme hata siku moja hatosheki na mwanamke mmoja ukweli ndo huo
japo mnaufumbia macho halafu wewe unanishangaza eti hujaolewa unatokwa na povu
la mdomo la nini sasa?! si ubakishe pumzi zako kwa yatakayo kukuta! ngoma si
yako waivalia kibwaya? muongo mkubwa! ushatendwa huko unaleta mihasira yako
hapa!
MWANAMME KIZUKA TU, AKIZUKA ZUKA NAE !!!

Nna kupa verse
hiyo:-

Kama unaweza mtie kamba mumeo,
ukitahamaki chini kachimba nnae
miyee, Nimeshamsombaaa Nnaringa nae,
tena Nnajigambaaa kama wangu miyeee!
Anonymous   |2010-03-16 10:40:54
NA WEWE MALAYA TU HUNA LOLOTE KWA UPUMBAVU WAKO UNAJISIFIA NA KUJIONA MJANJA
BADO HAYAJAKUFIKA SUBIRI UBAKI KILO MBILI... ULIEOMBA USHAURI HUNA AKILI WALA
HUJAFUNZWA WEWE,, UNAONAMOTO HUU ETI UNAULIZA HIVI NIKIGUSA NITAUNGUA? WAKATI
JIBU UNALO... ULEWA UONE... KWA TAARIFA YAKO HUYO KAKA KAKUONGOPEA KAMWE
HAMUACHI MKEWE NA WALA MKEWE HAJAKATAA KUJA DAR.. CHUNGUZA UTANIAMBIA..
Anonymous   |2010-03-15 23:33:33
KWELI...ILA LUGHA ULIYOTUMIA HAIFURAHISHI.WEWE MWALI...EMCHANGIA HIYO NDOA
KUVUNJIKA.NA HATA KAMA UNGEKUWA HUJACHANGIA...KEE ND'O UNAVIZIA HIVYO IVUNJIKE
UINGIE??HAA HAAA MAKUBWA!

kweli uahitaji usgauri?mbona uliishaafanya maamuzi
mapema sana?
Anonymous   |2010-03-16 02:34:21
duuuu, huyu dada inaonekana ana machungu sana .........
inaonekana ametendwa
...... lol
Anonymous   |2010-03-15 16:29:01
MMH USHAURI GANI SASA HAPO JAMANI! WAKATI WEWE KWA NJIA MOJA AU NYINGINE
UMECHANGIA KUVUNJA HIYO NDOA! ULIPOJUA KAOA.. UNGETOKA HAPO HAPO, LAKINI KWAKUWA
ALIKUWA NA WEWE, HAKUPATA PUMZI WALA NAFASI YA MAWAZO YA KUMKUMBUKA MKEWE,
UTAKUWA NA DOA BIBI 'KIMADA' SIKU ZOTE. JAMANI WANAWAKE WENZANGU ACHENI WATU NA
NDOA ZAO..., JANAMUME LIKIKWAMBIA LIMEOA BAADA YA KUKUDANGANYA MUOGOPE ! FIKIRIA
FAMILIA UNAYOIBOMOA, SIO KUCHANUA HAPO.
Anonymous   |2010-03-15 18:33:43
na wewe ukiolewa ataenda kut** nje huwajui hao hawabadilikiiii ilooooo utachekwa
bana miguu tulizana upate wako bibie shame upon u!
Anonymous   |2010-03-16 02:11:59
kaomba ushauri sio mjifanye mna hasira saana na kuanza kutukana wenzenu ovyo
sana kujisheua tuuu kama vile na nyie hamjawahi kutembea na waume za watu kwani
cha ajabu nini? mwanamme ndo alimtongoza mpeni ushauri kama mlichukuliwa waume
zenu kwa midomo yenu michafu huko huko oyaaa bidada eeh usiolewe naye huyo
tafuta wako wa kuishi naye ila endelea kurusha naye roho hadi upate wakwako
shostito   |2010-03-16 03:38:31
jamani tuangalie na upande mwingine wa shilingi. sometimes na sisi wanawake
tunachangia sana waume zetu kutoka nje ya ndoa. msimlauma sana huyo dada. huyo
mkewe kilichomfanya asije dar kumfata mumewe ni nini? halafu na yeye huko
anatoka na wanaume tena peupe mpaka ndugu wa mumewe wamejua hivi mnafikiria nini
hapo. wote vicheche mume na mkewe sasa sio mumhambulie dada wa watu.

hiyo
ndoa kudumu au kutokudumu wala sio sababu ya huyo dada kwanza keshawaambia kua
mwanzo hakujua kama kaoa wapo wanaume ambao wasiri sana na huwez kujua kama
kweli kaoa ukizingatia mkewe yupo mbali. mumpe ushauri mzuri sio kumtukana na
kumkashifu yupo njia panda ndio maana kaomba ushauri na kama amekosea kuna njia
nzuri na maneno ya kistaarabu tu ya kumrekebisha mtu sio kumtusi hakuana mtu
perfect wote tuna kasoro bwana

ni hayo tu kwa upeo wangu
Bigger  - Ms.   |2010-03-16 05:29:24
Kwa kweli dada, mimi ushauri wangu ni kwamba, huyo mwanaume hakufai kabisaaaa!
kwa sababu ni mume wa mtu hata kama ataachana na mke wake.

unasema kwamba eti
mkewe ana bwana huko kwao mwanza, mbona yeye ana bibi hapa dar es salaam ambaye
ni wewe?? acha kujishusa, kuona kwamba akifanya mwanaume sawa, akifanya mwanamke
ndio mbaya! wote wamefanya vibaya, na usifikiri kwamba kama huyo mwanaume hakuwa
perfect kwa mwenzako ndo atakuwa perfect kwako. hiyo never, na kama yawezekana
ni kwa wanaume wachache sana.

umefanya kosa kubwa sana kutembea na mume wa
mtu, kwanza kabisa huo siyo utamaduni wetu kama watanzania, ingawa wapo watu
wanaofanya hivyo, ila habari ndo hiyo. you need kurepeant na safisha hiyo, kwa
sababu always WHAT GOES AROUND, COMES AROUND. dhambi bibie

Big
Anonymous   |2010-03-16 06:06:49
mimi ni anonymous wa kwanza sina hasira yoyote wala sijawahi tendwa nina mpenzi
wangu na tunapendana sana ila umenikera sana kutuchafulia hali ya hewa humu
kwakutuletea mada ya kijinga badala yakujadili mambo muhimu.narudia tena wewe ni
malaya husband snacha na hao wanaokutetea wapo kama wewe huhitaji ushauri wowote
majibu unayo mwenyewe acha mume wa mtu katafute wako put it in ur mind.nyie ndio
wavunjaji wa ndoa za watu mnasababisha watoto wanakosa malezi bora ya baba na
mama.kama huyo mwanaume ameshindwana na mkewe waliokula naye viapo unadhani wewe
ndio mtawezana narudia tena unajidanganya mwenyewe go and look for ur own
husband kama unataka kuishi maisha ya amani acha kujitia vigundu visivyokua na
ulazima nafasi bado unayo umeshajua ni mume wa mtu achana naye.najua ukweli
unauma na watu hua hawapendi kuambiwa ukweli wanataka kudanganya .lakini huo
ndio ukweli take it or leave it
Anonymous   |2010-03-16 10:46:34
well said my dia... dada msikilize huyu mmwenzio hajaolewa lakini ana busara na
anaona mbali... ungekuwa hauna boyfriend walah ningekutafuta nimuweke kaka yangu
lol!
Anonymous   |2010-03-16 06:15:53
hivi wewe dada una akili zote kweli wewe?nahisi unakaupungufu ka akili sio
bure
eti mkewe kakataa kuja kuishi Dar na mumewe,wewe inakuhusu nini hayo ni
mambo yakifamilia na hiyo sio tiket yakumjudge huyo mwanamke nakuona ni sawa
wewe kutembea na mumewe.Hivi wanawake tunatatizo gani.katafuta mumeo acha
kujitia shombo na waume wawenzanko.kama unajua wanaume hawatosheki basi na wewe
jua siku sinyingi atakuacha
Anonymous   |2010-03-16 07:07:04
kwendeni zenu huko, nani kakwambia kutembea na mume wa mtu ni kujitia mikosi?
hovyooooooo, nyinyi ndio mnashindwa kuwazibiti waume zenu harafu wakitoka nje
mnaanza kulalama, nani kakwambia mme wa mtu sumu? hivyo ni vineno vyenu tu
mnavyojitungia na kujiliwazia, mume wa mtu ni sawa tu na mwanaume ambaye hajaoa,
wote wakko sawa tu, hivyo nakushauri dada yangu, kama kakufuata mwenyewe mpe
kitu roho yake inapenda, ata kama anataka kukuoa olewa nae tu huyo ni mwanamme
kama mwanaume mwingine tu ambaye hajaoa. wewe dada uliyetoa ushauri mwanzoni
naomba namba ya mmeo kama hautojali.
Bigger  - Ms.   |2010-03-16 09:41:34
WHAT GOES AROUND, COMES AROUND BIDADA. BE CAREFUL
Anonymous   |2010-03-16 10:50:22
dada nyie mnaotenbea na waume za watu ndio mnamatatizo tena makubwa... kama
kweli mko kamili kwa nini hampati wa kwenu fresh!... haloooo mtato**a sana mpaka
K zichakae then wanarudi kwa wake zao nyie mnakalia kuhangaika huku na kule kama
mbwa koko na kuzeeka wapweke...
Anonymous   |2010-03-16 07:11:13
ANONYMOUS WA KWANZA NAOMBA NAMBA YA MMEO KAMA HAUTOJALI. HAHAHAHHAHA HAHAHHA,
YAANI NIMECHEKA MPAKA BASI, WEWE ANONYMOUS WA KWANZA UMEINGIA NA JAZIBA UTAZANI
NDIO UMECHUKULIWA MMEO, HAHAHAHAA, UKIWA NA PUPA NAMNA HIYO UTACHUKULIWA NA
WAKWAKO, MME NI MTU TU WA KAWAIDA KAMA ANAUME WENGINE AMBAO HAWAJAOA, HIVYO DADA
ZANGU MSIPENDE KUWASHOBOKEA NAMNA HIYO WAUME ZENU, NA UKAE UKIJUA HAKUNA
MWANAUME WA KWAKO PEKE YAKO HAPA DUNIANI, ENDELEA KUMCHUNGUZA MMEO UTAGUNDUA TU
KUWA ANA KIMADA KINGINE ZAIDI YAKO WEWE UNAYEJICHEBEDUA KWENYE NDOA, HAHAHHAHAHA
MWAKA HUU MNALO WANA NDOA.
Anonymous   |2010-03-16 10:54:28
walioolewa hawajishebedui dada kumbuka mwisho wa siku lazima ile kwa kimada pia
taha huyo mungu alie juu anaangalia na kukasirishwa kwa hiyo hasira ya mungu
pekee utajuta kuzaliwa.. kwanza yote ya nini lol.. bora nijitafutie wangu
mwenyewe bibi akiwa na mwingine mwizi ila mm ndio mmiliki...
Anonymous   |2010-03-16 07:16:08
anonymous wa kwanza husiwe na jaziba jamani, mi nakushauri uwe unamweka mmeo
kwenye pochi ukiwa unaenda kazini ili muda wote uwe nae, hahahahhahaa unaogopa
kulambiwa eeeeeee, muweke kwenye pochi yako uwe unaenda nae kila utakapokua
unatoka home kwako, lakini kama uwezi kumweka kwenye begi lako ukiwa unatoka,
basi waacha watu wajivinjali nae, wewe unamvamia dada wa watu eti malaya,
malaya ni wewe, kwa nini usimvamie huyo mwanaume aliyemtongoza na uku akijua
ana mkewe? dada wa watu katongozwa, ata ningekua mimi ningeruka nae tu yeye si
ndie aliyenitongoza? kwani yeye kamwita aje kumtongoza?
Anonymous   |2010-03-16 08:31:51
wewe dada ulieta hii mada na nyie woote mnaom sapoti na kumponda anony wa kwanza
wote mna upungufu wa akili...ww unaeomba ushauri jua kuwa za mwizi ni 40 na kaa
ukijua kuwa kama ameweza mtosa mkewe for u nxt time utatoswa ww kwa ajili ya mtu
mwingine,watch out kwanza i hope mmepima ma it might be that jamaa ana ngoma,kam
akweli utaendelea na uyo mume wa watu ombi langu mungu akuadhibishe accordingly
Anonymous   |2010-03-16 10:56:24
kweli kabisa waeleze
Anonymous   |2010-03-16 08:53:14
Mume wa mtu mtamu jamani! Nyie acheni tu!
Anonymous   |2010-03-16 08:58:28
hahahhahahha
mnanifurahisha kwelikweli ukweli umewaumae mahusband snachaz
mimacho imewatoka kwa haya mmekua manunga mnahamia kwawaume za watu
lol hebu
msinipotezee wakati mie
hahahhaahhaha
mnalo Manunga embe
Anonymous   |2010-03-16 09:04:35
jamani mie anonymous wa kwanza wala sijaolewa ilatu huyu kanikera na hii mada
yake wala sina hasira.nyie mnaomsapot mnakaupungufu kaakili sio bure
tena
mwanifurahisha kweli mlivyofura kwakuwaambia ukweli lol
mnalo katafuteni waume
zenu.huo ndio ukweli take it or leave it.kaukweli kanaumae.
hahahahhaha
hebu
cheki masnacha yalivyo fura kwa hasira na uchu mimacho imewatokaa
Anonymous   |2010-03-16 11:02:23
Wape wape vidonge vyao mdada... kwa utafiti wangu kweli waume zetu wanapotoka
nje tuwe wapole na kuwarudisha cheki watu walivyo na hasira kisa manungayembe
unadhani akikutana na mumeo huyo inakuwaje?!! mijitu iko desparate na waume za
watu koz hawauziki lol kwa ujinga wao wanapendwa kumbe wanatumiwa haloooooo
UTAKUWA NAE LAKINI USIKU ANARUDI KWA MKEWE WANAKUMBATIANA HADI ASUBUHI WEWE
UNABAKI BARIDI LAKO MITO YAKO AU UKISHIDWA WALALA NA YOYOTE TABU YOTE YA NINI??
Anonymous   |2010-03-16 09:06:10
Mimi niligundua mume wangu anatembea nje ya ndoa na nina mimba kubwa ya mtoto wa
pili. Kwa upelelezi wangu niligundua huyo nyumba ndogo anajua sana kuwa mume
wangu ana mke na mkewe ana mimba. Nilichomfanyia huyo dada, sidhani kama
atarudia kutembea na wame za watu. Ilibidi anilipoti polisi japo haikumsaidia
kwani even my husband was on my side. He was not real in love but nyege tu due
to mya pregnance. Wadada wa nje nyie ni vipoozeo tu mnajitia nuksi mtabaki
madunga embe. Huyo dada niliforward e mails kwa rafiki zake wote kuwaharifu
uchafu wake na nadhani ndiyo ilomuuma zaidi kwani walidhani ni decent fulani and
may be among the addresses kuna wachumba. She is 35 almost my age na ana shape
ya kibantu lakini naweza sema kadoda sababu ya uchafu wake wa tabia
Anonymous   |2010-03-16 09:37:59
Mimi sijaelewa mbona mmesema hakuna mwanaume asieenda nje alafu mnamwambia huyu
dada akatafute wa kwake!atajuaje kama huyo wa kwake ni wa kwake kweli?maanake mi
ninachojua kila mtu ana mtu wake hata kama hajaoa anakua na girlfriend mpaka
umpate lazima umtoe kwa mtu!haya mambo yapo complicated sana!
Anonymous   |2010-03-16 11:15:45
mwache huyo mwanaume hakufai kbs tafuta wa kwako mume wa mtu ukishakuwa nae ni
laana waweza kuta mkewe amegungua kuwa jamaa ana mwanmke dar ndio maana na yeye
anaamua kumvunjia heshim.so kwa upande mwingine wewe ndio unavunja ndoa ya watu.
naweza kushauri mambo mengi lakini cha msingi ACHANA NAE HARAKA.Kama ni mwislam
basi akuoe mke wa 2 na umsihi asimwache mkewe maana ndoa ikishakuwa na mtoto
kuivunja kwa tamaa za kidunia ni mbaya (dada ushauri)
Anonymous   |2010-03-16 11:18:49
upumbavu tu
sasa ushauri gani unataka wakati tayari umeshafanikiwa kuvuruga
ndoa ya mwenzio
hujui kama wewe ndio sababu
hebu kula kona,,na acha kumtesa
mwenzio kama matatizo ni yake na mumewe wewe hayakuhusu.JIHESHIMU
MWANAMKE,THAMINI MWILI WAKO.HAKUNA KITU KIZURI KAMA KUA NA MUME WAKO PEKE
YAKO.............USIPOTEZE MUDA NA MUME WA MTU..MUME WA MTU NI WA MTU
TU........
PUMBAVU!!!!!!
inaonyesha una uwezo mdogo sana wa kufikiri hizo
story zote unazopata ni za kukushawishi wewe uolewe sio za kweli na hata kama ni
za kweli hazikuhusu.&believe me utaolewa kwa miezi 3 tu utaanza kujuta.next time
usituwekee huu upumbavu
Anonymous   |2010-03-16 11:23:22
wenye upungufu wa akili ni hao waume zenu walokula viapo vya kutotembea nje ya
ndoa lakini bado tu chupi mkononi mtashaa yani mume wa mtu akinitongoza kwa raha
zangu najiachia naye hadi kwenye kitanda chake na mkewe kwani mie na tofauti
gani mkewe? nilishafanya hivyo na nadumisha hii mila wanawake tuko wengi duniani
kuzidi wanaume sasa sie tukarushwe roho na baba zetu au?? nyambaff tutabanana na
nyie hadi mtie akili acheni choyo ebo!! kwanza mume wa mtu mtamuu unaruushwa
roho kivingine unadekezwaaaaaaaaaaaaa kama nyau he he haloo mtajijei jei
tubanana hapa hapa tule mkono kwa mkono kama we wa nyumba kubwa mie wa nyumba
ndogo!
Anonymous   |2010-03-16 11:26:24
MME NI MTU TU WA KAWAIDA KAMA ANAUME WENGINE AMBAO HAWAJAOA, HIVYO
DADA
ZANGU MSIPENDE KUWASHOBOKEA NAMNA HIYO WAUME ZENU, NA UKAE
UKIJUA HAKUNA
MWANAUME WA KWAKO PEKE YAKO HAPA DUNIANI, ENDELEA
KUMCHUNGUZA MMEO UTAGUNDUA TU
KUWA ANA KIMADA KINGINE ZAIDI YAKOWEWE ULIEANDIKA HUU UTUMBO YOU ARE NOT FINE KICHWANI KWAKO.......I MEAN
NI
WALE WADADA WALIOKATA TAMAA YA MAISHA WAMEBAKI KUZURURA TU MTAANI POLE
ZAKO!! SALI MUNGU ATAKUJALIA UTAONDOKANA NA MAWAZO
HAYO POTOFU..
HEEEEE
TAJIJUUUUUU
Anonymous   |2010-03-16 11:28:14
basi mkaka akaona hapa ndiyo safi akaniambia kuwa anataka kunioa mie na yuko
serious .......A
ACHA UPUMBAVU
Anonymous   |2010-03-16 11:36:49
wewe anonymous wa kwanza nimesema naomba namba ya mpenzi wako jamani.
Anonymous   |2010-03-16 11:39:04
HIVI NGOJA NIULIZE SWALI, MBONA WANAUME UWA HAWANA KIPINDI CHA KUWAGOMBANIA
WANAWAKE? AU KUMKUTA MWANAUME NA MWANAUME WANASEMEZANA KUHUSU MWANAMKE, SISI
WANAWAKE TUNAWASHOBOKEA SANA NDIO MAANA WANAUME WETU HAWAISHI KUTUFANYIA VITUKO
KILA SIKU, JAMANI JIFUNZENI KUPUUZIA HAWA WANAUME, TUSIWE NA VIPINDI VYA
KUWAGOMBANIA NAMANA HII WATATUTESA SANA
Anonymous   |2010-03-16 11:45:48
waume zenu hata muwafungie kofuli ya viro watatafuta master key wazifungue yani
nyinyi wanandoa inabidi mtuheshimu sana sisi mamistress tunasaidia ndoa zenu
zisivunjike kubalini mkatae huo ndo ukweli wenu tunajua kuwatoa hao mamista wenu
stress mnazowapa kwa ajili ya mikelele yenu uchafu gubu mnajiacha ovyooo wengine
mwanuka vikwapa midomo nako tunako yani mna fedheha nyinyi hamjui tuu basi
tunawaombeaga msiachwe hamjui hilo ngoja niwaambieni hawa wanaume zenu
wanawapenda tatizo nnyie hamuwajali mnajifanya kama kaka na dada wakija kwetu
full masaji jamani almanusra nivunje ndoa ya watu kisa masaji tu mh ikabidi
nimuache yule baba nyie acheni tuu kuweni wabunifu sio kupika wali nyama kisamvu
mkadhani inatosha na mpunguze midomo huwa tunalalamikiwa sana na kulalamika ovyo
mume wa mtu ni kiburudisho cha mtima
Anonymous   |2010-03-16 15:37:24
subiri na wewe uolewe kama utaweza kufanya hayo masaji. Wanaume wanaudhi mnooo..
unafurahia kwa kuwa unakutana nae part time!
Anonymous   |2010-03-16 11:58:00
anon wa kwanza hajaolewa ila ana boyfriend ! msituletee hapa watu wana toka na
kina jay z tiger woo denzel clinton kina brad pitty hadi wakavunja ndoa zao ndo
iwe bongo wanaume bwana babao mmoja tuu ni sawa na mbwa dume akiona jike ni
kunusa tuu hivyo kuwekwa ndani si tija ishu ni hao wanaume hata sie tusokuwa na
ndoa tuanajua wazi hata sie waume zetu watakujacheat sana tuu manake tunakaaga
na waume zenu wanatongoza mabinti wa watu hata wakikataliwa wanang'ang'ania
utadhani luba mara ooh nitafutie jamani awe kama wewe yani waume zenu wana visa
kwa hiyo avunjaji wa ndoa zenu ni waume zenu ambo ndo watongozaji wakuu
Anonymous   |2010-03-16 12:14:25
wewe dada ebu achana na huyo mume wa mtu, tafuta wako, kama huwezi kupata
wasiliana na mimi ninamarafiki wa mme wangu kibao ambao wanatamani kweli kuoa
wasichana wa kitanzania, kama unapenda wazungu I will hook you up with
one......

mdau
UK
xoxo   |2010-03-16 21:03:16
SIKILIZENI NYINYI HATA KWENYE BIBLE IMEANDIKWA KWAMBA WANANDOA WANAWEZA KUACHANA
KAMA MMOJA WAO AMEDHINI NJE YA NDOA SASA BASI HAO WOTE MAMEDHINI NJE YA NDOA KWA
HIYO KUACHANA SIO KOSA LAKNI INABIDI MWANAMUME ATOE TALAKA NA MWANAMKE ATAFUNGA
NDOA KAMA KAWAIDA NA HATA MUNGU MWENYEWE ATAIPOKEA NDOA YAO KWA HIYO DADA YANGU
WALA USIJALI MANENO YA WATU HUO NI USHAURI WANGU HATA UKIENDA KANISANI
UKAMUULIZE MCHUNGAJI WAKO .LKN PIA MUNGU HAPENDI TALAKA HILA KAMA MMEDHINI NJE
YA NDOA TALAKA RUKSA...KWA HIYO DADA NARUDIA TENA WEWE OLEWA TU.KUFUNGA NDOA SIO
KUISHI DAIMA MILELE WAMEFUNGA NDOA KINA USHER ,KINA J LO ETC ETC NA WALIACHANA
NA NDOA ZAO SEMBUSE HUYO MWANAUME
Anonymous   |2010-03-17 06:58:15
WANA NDOA OYEEEEEE, KIDUMU CHAMA CHA NDOA, KIDUMU. HAAHAHAHHAHAHAHAHAH, MNALO
LIMEWAGANDA WANA NDOA, LAZIMA TUWAZIBITI NA HAO WAUMEZENU. HAHAHAHAHHAA, MME WA
MTU MTAMU JAMA. HAHAHHAHAHHA. WANANOGEWA NA SISI NYUMBA NDOGA JAMANI, KWA HIYO
TULIENI TU MAJUMBANI MWENU, NYIE SI MMEOLEWA? SASA KELELE ZA NINI?
HAHASHHAHAHAHAHHA , HALO HALOOOOOO
Anonymous   |2010-03-17 11:11:40
sasa wewe mdada, huyo mwanamke huko mwanza ndio katia aibu maana ana bwana,
lakini nyie huku Dar MWATOA aibu, au nisemeje jamani? mimi sioni kama kuna ndoa
hapa, hapa ni kudanganywa tu mdada kama ilivyo kawaida ya hawa wababa, I love
you kibao, kwa kila anayekutana nae. achana nae, kwani umekosa nini hadi uolewa
na 2nd hand! inahusu nini, kitendo cha kua na mume wa mtoto ni kosa tayari na
dhambi kwa mwenyezi mungu. hata wewe utaachwa tu kama mwenzio, mwenye tabia yake
haiachi, usijione umefika mwanamke. mteme huyo ni muoaji uendelee na maisha
yako.
white  - Ms   |2010-03-17 11:45:31
Kwanini usitafute wako. Be in her position, ungefurahia kufanyiwa hivyo kweli
ndio maana hatuendelei hata siku mmoja. VAA KIATU CHAKE NDIO UTAJUA UCHUNGU
ANAOPATA MWANAMKE MWENZIO.Its high time nasi kuonyesha sio wa kuchezewax2
Anonymous   |2010-03-17 14:21:34
Hee hee halo halooo! Haloo ya vimada, halo; hallo wa wenye ndoa halloooo!

Mabinti kweli mnachekesha eti mume wa mtu mtamu, je wako mchungu? Maana na wewe
iko siku utapata wako utatendwa dada. Sasa kama huyu binti masikini ya mungu
pengine tayari ana mimba, ndio ana mshawasha wa kuolewa.

Halafu na huo
mzunguko sijui kama kuna kupona ukimwi hapo, maana mume anapeleka mkia wake
hovyo na mke naye anatembeza kifuu chake cha nazi kikunwe, kisha wanakutana mke
na mume, kisha na wewe unakwenda kuingia kwenye huo mduara, kweli Tanzania bila
Ukimwi Haiwezekani.

Ushauri wa kwanza kapime ngoma dada, huyo sio mume ni
gume gume lilowashinda mitume!

Hiyo part one subiri part two
Anonymous   |2010-03-17 14:28:45
Part two!
Mie umri wangu ushaenda lakini sikuwa namtia kamba mume wangu wala
nini, niikuwa namwambia wewe dini inakuruhusu unatakana kukuna nazi nyingine,
kaoe niko radhi, ila usinitie dhambi ya Zinaa kwa kusema nimekukataza kuoa aah
mie sina tatizo na ukewenza, kaoe baba kaoe usijeenda kuzini. Na ukizini ni lako
peke yako, halafu nauchuna naendelea na shughuli zangu simfatilii mambo yake
kabisa. Ila nilimwambia nikikuta na kimada ndio mwisho wa hii ndoa kwa sababu
huna sababu ya kuwa na kimada.

Huu mwaka wa 20 sasa, hajaoa wala hana mpango
wa kimada wala ndoa. Na wako VIBIRITI UPERE walokuwa wanajaribu kujiepelekesha
kwake, mara sijui msg nakuhitaji, sijui nakumiss. Nilichokuwa nafanya, usiku
napiga simu majumbani kwao, bahati mbaya zinapokelewa na wanaume /boyfirend zao,
nilikuwa nawaambia tu jamani mume wangu ni Muathirika mkanye huyo dada asije
ambukizwa bure!
Anonymous   |2010-03-17 14:51:01
Wewe anonymous wa kwanza, cjui utawaadhibu vp watoto wako...hata kama umeona
kweli huyu dada ana makosa.cyo kum2kana kiivyo..mpaka wa2 wanahisi
imekugusa..nway inaweza ikawa imekugusa but find gud words 2 tok 2 ur
blogmet...afta ol ameomba advice..na kumbuka she is in love wether amekosea au
lah...onya mtu but HAVE GUD TONE.
Bibie...mwanaume umuache,wat goes around comes
around,hata kama ana matatizo na mkewe,.usiwe chanzo..acha aachane naye..but we
ukiwa pembeni, if u guys ment 2 b 2gether samdays huko, hata ukipata boyfrend
now...mnaweza mkaja achana n in lyf ukajikuta unarudiana na huyo mume wa
mtu(akiwa single officially).
tho i do pray n plz do pray too upate wako.
Mungu
anasema mwanamke anayetoka na mume wa mwenziye ni shetani.....are
u???????????
Plz stay aside. mshirikishe Mungu sana coz Peke yako hauwezi.
Write comment
Name:
Email:
 
Website:
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
:angry::0:confused::cheer:B):evil::silly::dry::lol::kiss::D:pinch:
:(:shock::X:side::):P:unsure::woohoo::huh::whistle:;):s
:!::?::idea::arrow:
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

 
 
U Turn Polls
Wangapi mnapenda U-tun ibaki hivi hata kama Mama u turn akifungasha Virago?
 
ADS Only