17April

DAH SIKU YA LEO.....UMESHAWAHI KUPITIA KITU KAMA HIKI???

So siku ya leo nimeanza nayo vizuri ila imeishia vibaya....

At around 12pm I went to the grove kununua sunglasses zingine maana zile nilizovaa jana Kenzo alizikalia jana usiku...

Baada ya hapo I thought ngoja niwe mama mzuri nkawapeleke watoto to the park, so i went back home ,nkamwambia dada hana haja ya kusubiri mpaka 6pm leo asepe zake tu, nkawabeba wanangu wote.Wakati tuko njiani tunaenda kwenye park nkaona niwanunulie watoto drinks and snack wanywe tukiwa park, basi nikasimama kwneye petrol station.

Kumbe nimeshuka kwenye gari nimeacha gari kwenye neutral na sio P. ile nimeingia petrol station tu naskia mtu anapiga honi kama kachanganyikiwa nikaangalia nyuma, uwiiii gari yangu ilikuwa inarudi nyuma yenyewe na wanangu wapo strapped in their car seats ndani ya gari,

kumbe msamaria mwema aliona gari lilivyokuwa linarudi nyuma ndo akawa ananipigia honi. Nilidata, acha nitoke mbio, sijawahi kimbia hivyo in my entire life, ila sasa mwili haukunipa support kwa vile sijakimbia wala kufanya zoezi kwa miaka kadhaa basi nikadondoka chini, PUH, kama gunia vile, tena nimeangukia uso kabisa....Ila sikusikia hata maumivu ya kudondoka nikaamka fasta nikaanza tena kukimbiza gari langu, hapo tayari watu wengine waliokuwa petrol station wamepanick, kuna wanaopiga kelele, kuna wanaokimbiza gari na mimi, yani kama movie vile. Alafu sasa gari linarudi nyuma linaelekea kwenye pump za mafuta. Mungu ni mwema ,yani right before the car hit the pump nilifanikiwa kufungua mlango na kuruka ndani ya gari and hit the brakes. actually kwa kiwewe nilichokuwa nacho sikukumbuka hata ipi kwa zile pedal 3 ni break, I think nilikanyaga ya kwanza ikawa sio ya pili ndo nikapatia... Hapo Kenzo na Bhoke wana scream vibaya mnoooo....

Kuna waliopiga simu 911 tayari yani It was chaos....... Ila i have to admit jamani wenzetu nchi hii wanajua kusaidia jamani, yani watu walivyokuwa wnakimbiza gari na mimi utadhani ni watoto wao humo ndani....

mama mmoja akaanza kulia anasema anahisi kama ni wanae ndo walikuwa kwenye gari...

Basi nikaingia kwenye gari nkwaambia wanangu tunanenda nyumbani  coz of what happened , also because nimeumia ,maana nimechubuka goti,mkoni na elbows zote mbili zimechubuka, Kenzo akatiaje "Noooooo, get my drink first", yani na maumivu yote ilibidi nicheke, watoot jamani imagine bado anataka drink yake, nikashuka, nkaingia petrol station huku natetemeka kwenda kumnunulia hiyo drink, maana alianza na kulia anataka his drink, nimeingia petrol station watu wananiuliza ' OMG you are still buying the drinks' nikawaambia My 3 yr old haelewi anataka drink yake, acha waangue kicheko, yani ilibidi kila mtu acheke.....


iM STILL JUMPY, I NEED TO CALM DOWN......

Kuna mliowahi kupitia kitu kama hiki???? what did you do???

Yani kuanzia leo kabla sijashuka kwenye gari ntakuwa naangalia mara kumi kumi kuwa gear ipo on P....

16April

3RD TIME MOMMY TINGZ......

Leo nilienda Farmer's market /The Grove for some nyama choma na kunyoosha miguu na new baby......

Kitumbo kimekwisha ila nanenepa sasa...lol..

Mie kikawaida ni mtu mnene, yap kama sio madiet yangu ni mtu wa kuvaa size 12-14 huko..... So now vile no diet mwili wangu ndo unakujaaaa haswaaaa.....

Ila sina haraka na mwili mpaka mtoto aache nyonyo.....lol...

 

 


16April

TELEX FREE FILES FOR BANKRUPTCY IN THE US.......

Siku mbili zilizopita telexfree wamefile for bankruptcy marekani.....

Maskini sijui waliokuwa wamewekeza nao huku marekani wana hali gani,,,, maana mtu akifile bankruptcy huwezi mdai deni.....

Mliotusikiliza huko bongo mkaachana nao hamkukosea.....

Kwa habari zaidi ingia humu....

Na humu


14April

POLENI KWA MAFURIKO......

 

 

 

 

Hata uzunguni ni balaa vile vile.....

 

Dah, poleni sana ndugu zetu mlioko Bongo kwa mafuriko...... Badala ya mvua kuleta neema imeleta balaa.....

You are in our prayers........

12April

UZEE MWISHO CHALINZE... ASHA BARAKA AOLEWA!!!!

Asha Baraka akiwa na mumewe kwenye Aqdi jana

 

 

Mama Keanu naona blog inachechemea kwa uzazi habari ya mujini hiyo nakuletea

Asha Baraka kaolewa jana (Ijumaa) harusi ya siri hakuna mwenye picha hata magazeti ya udaku hawajapata, nimekutumia wewe kwanza

sababu naipenda sana blog yetu.

Wanawake wenzangu tusivunjike moyo tunapokosa wachumba ujanani, hata uzeeni waweza olewa na ukaishi maraha ya raha na mumeo, mfano halisi ndo huu wa Asha Baraka.

Hongera Asha kwa kutuletea baba.

11April

USIKU WA MNYAMAAAAAA........ NI T.I.D.............

Usiikose hii...... Itakuwa POA SANAAAAAAAAAAA.........