|
Hi Mange, pole na kazi na asante sana kwa habari na entertainment tunazozipata kwenye blog yako pamoja na udaku, i love ur blog by the way am a huge fan.
Mimi leo niko radhi wadau wanishambulie lakini uzalendo umenishinda nataka ushauri maana nataabika. Mimi ni mwanamke wa miaka 31 ninaishi mwenyewe, nina elimu nzuri na nimebarikiwa kua na kazi nzuri sana, nipo single na nimetokea kumpenda mwanamke mwenzangu sana, ni mdada ana umri kama wangu. Yaani nikiwa nae naenjoy sana, we have so much fun, tunasaidiana na tunaenjoy sex mno, ananipa mapenzi ambayo sijawahi pata toka kwa mwanaume yeyote, i'm inlove with this woman so much. Hali hii sio kwamba imenianza leo wala jana, ni muda mrefu navutiwa na wanawake wenzangu, guess I'm a lesbian. Watu wananishangaa inakuaje dada mzuri hivi hana mwanaume??wangejua naumia kiasi gani. Sasa hivi nimetokea kumpenda huyu dada, nimempenda kwa mapenzi ya kweli kama mpenzi wangu na yeye ananipenda mno, tumekuwa wapenzi kwa muda wa mwaka mmoja sasa, najua kama binti wa kitanzania sitaweza kua nae milele, lazima ataolewa, nalia kila siku nikiwaza hilo na sina jinsi zaidi ya kukubali huo ukweli, nimejaribu kila njia ya kujibadilisha nimeshindwa, nimejaribu kudate wanaume nashindwa kua nao kwa muda mrefu maana navutiwa zaidi na wanawake. Sasa huyu dada ni majuzi tu ameniambia ananipenda sana lakini kijamii lazima awe na boyfriend ili aweze kuolewa maana familia yake sasa imeanza kumuulizia hiyo issue na tayari kuna mwanaume amemtaka urafiki, anadai hampendi coz moyo wake uko kwangu lakini hana budi, i believe her sababu naona anavyotaabika na suala hili pia, nimelia sana juzi alivyoniambia hivyo, na yeye anaumia mno hataki tutengane. Siju nifanyeje maana tunapendana sana na siko tayari kumpoteza, ni vigumu mtu kuelewa naumia kiasi gani mpaka uwe kwenye situation kama yangu, sasa hapa nilipo sijielewi nifanyeje, ye mwenyewe kachanganyikiwa, kwao wanamuuliza vipi unaolewa lini hana jibu, sasa sijui ni end vipi hii r'ship nae, jamani naogopa kuumia na yeye anaogopa kuniumiza but it looks kama hivyo ndivyo itakavokua, i don't wanna let go, i'm confused, help, nitashukuru kama wadau watanishauri, mkinijudge nitaelewa coz kwenye jamii ya kitanzania sikubaliki but i can't change who i am, i love women and there's nothing i can do about it.
Asanteni,
-Kathy-
|