Who's Online
We have 386 guests and 1 member online
  • Fleetaves
Total number of Visitors
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday6683
mod_vvisit_counterYesterday8768
mod_vvisit_counterThis week6685
mod_vvisit_counterLast week82441
mod_vvisit_counterThis month53757
mod_vvisit_counterLast month319970
mod_vvisit_counterTotal No. since we started4933324
Login



KUMBE INAUMA JAMANI....
Written by Mange   
Tuesday, 30 March 2010 22:01

Hi Mange,

Ningependa ku-share na fans wa wa U-turn kujua jinsi gani wanawake tunatakiwa kuwa.

Nilikuwa na mume wangu wa ndoa na ndoa yetu ilifika mwaka mmoja tu. Mimi nilikuwa nafanya biashara yeye ni mfanyakazi na katika ndoa yetu tulikuwa tunapendana sana lakini bado tulikuwa hatujabahatika kupata mtoto.

Nilkuwa nimekwenda South Africa kwa ajili ya bihashara zangu nikiwa huko zilikuwa zimebaki siku chache nirudi tanzania na pia nika plan nirudi siku ya 1st Anniversary ya ndoa yetu ila nichokifanya siku moja kabla nikamwambia hubby kuwa nimekosa flight ya kesho yake hivyo nitakuja the next day basi akasikitika sana maana tuliplan nikifika tutoke out.

ila kumbuka kuwa niliamua kumdanganya nimfanyie suprise hubby wangu. Basi siku ilipofika nikarudi na nilipofika airport nikachukua tax ile nafika home mlinzi kanipokea nikamuuliza kama hubby wangu yupo akasema yupo nikaingia ndani straight nikaenda chumbani ile naingia chumbani nilimkuta hubby na mwanamke wote wpo kama walivyozaliwa.

nilichofanya ni kutoka pale nikaenda guest room nikavua nguo nikaoga nikatoa nguo zangu nilizoandaa kuvaa siku hiyo na suit ya hubby niliyomletea ili avae nikaziweka vizuri baadae kidogo mume wangu akaja chumbani nikamuuliza kama mgeni wake kaondoka basi akajibu kaondoka nika m hug na nikampa suit yake nikamwambia jiandae tutoke maana ni anniversary yetu basi tukatoka out tuka enjoy na tuliporudi home nikampa hata haki yake pia.

Siku zikaenda hata miezi ikatika siku ya siku ya siku ikafika. Nilikuwa na mdogo wangu wa kiume anaishi Nairobi ambaye hajawahi kuonana na shemeji yake nilimpigia simu nikamsimulia yote yaliyotokea nikamuomba aje Tz kwa ajili ya kumuonyesha inauma vipi. Mdogo wangu kweli akaja nikampokea nikampeleka nyumbani kwangu nilikaa nae mpaka nilipoona muda wa hubby kurudi tukaingia chumbani akavaa bukta yake kifua wazi na mie nikavaa khanga nyepesi moja tu tukajilaza kitandani akaweka kichwa chake kwenye mapaja yangu. Basi muda ulipofika hubby karudi home akaingia mpaka chumbani ile kufika tu pale kaanza ugomvi akataka kumpiga mdogo wangu kwa kweli mdogo alikuwa na hasira naye sana alimpa kichapo sawasawa basi akatoka nje mdogo wangu. Hubby akanza kulalamika akasema eti anatoka anakwenda kuwachukua wazazi wangu na mie nikatulia kimya nikampigia mdogo wangu nikamwambia asikae mbali na home basi jioni kwenye saa 1 hivi wakaingia pale baba, mama na dada zangu mpaka ndani.

Mashtaka yakaanza alipomaliza kuongea nikamwambia naomba undelee na yale ya kwako yote uyaseme pale akinama chini kimya nika mwambia mbona huelezi siku nimetoka South ilikuwaje? Kimya basi nikawaambia jamani mwanaume niliyekuwa nae msubirini anakuja muda si mrefua akaingia mdogo wangu wote wakashangaa kumuona pale.

Ikabidi nitoe story yote kwa kweli yule mwanaume aliomba msamaha sana.

Wadau tusiwe na papara na hawa wanaume tuwe tunawachukulia taratibu au tusifikie kugombana wenyewe kwa wenyewe maana tutazidi kuchukiana.

Thanks

Mdau

Comments
Add New Search
Anonymous   |2010-04-02 09:18:37
mange hebu uwe unatuwekea hadithi za kweli,hizi zakutunga achana nazo. hiki kitu
hakiwezekani kabisa kwa watu wenye ndoa changa hivi.
Write comment
Name:
Email:
 
Website:
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
:confused:8):lol::x:P:oops::cry::evil::twisted::roll::wink::!:
:?::idea::arrow::blink::dead::coffee::karate::gossip::hahaha::newpost::love::lips:
:no::nono::rofl::shrug::stop::tape::thumbsup::wail::waves::yahoo::yes:
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

 
 
Find U turn Blog on facebook