|
Written by Mange
|
|
Sunday, 28 March 2010 22:01 |
|
Yes dada mambo vp?
kwanza nakupa pongezi za dhati kwa kazi kubwa unayoifanya ya kuelimisha jamii, ki ukweli kwa hili unastahili BIG UP sana.
Jana nilikuwa naangalia ni kitu gani umetuwekea cha kuchangia, katika hayo kuna hili ulilouliza ni kwa nini Blogu yako imekuwa inapata watu wengi kila uchao.binafsi nina sababu nying tu lakini nitaelezea hizi chache ambazo mi naona ndo za msingi.
KWANZA: Mambo unayoweka humu yanaigusa jamii moja kwa moja na ni matukio yanayotokea kila siku;ama ndani au nje ya nchi bila woga wowote.
PILI:.umeweka uwanja mpana sana wa majadiliano au michango toka kwa wadau bila kuharibu mada iliyopo na hapa pia napenda kuwapongeza sana wadau wa blogu hii.kwangu mimi ubora wa blogu unaonekana kwa wingi wa comments tena karibu zote zikiwa zimekwenda shule.na pia ipo zaidi kwa matukio yanayowagusa hasa vijana kila siku.
Mwsho naomba nisaidie ni jinsi gani nami pia naweza kutoa comments kwani nimejaribu lakini naona sijafanikiwa.
NAKUTAKIA KAZI NJEMA
Mdau
James.
N/B nipo online.
|