Hi Mange!
Mimi ni binti naishi Dar es Salaam.. Naombeni ushauri wenu wana U turn.
Mimi nina boyfriend na tunakama miezi mitatu toka tuanze mahusiano yetu.. Boyfriend wangu ni mtu mwenye umaarufu kidogo hapa bongo kwasababu ya kazi anayoifanya inamkutanisha na wasanii na watu wengi. Kipindi ananifuata alinieleza kuwa alikuwa na girlfriend wanaishi wote kwake lakini wameshindwana tabia na kuachana. Siku niliyokwenda kwa yule kaka kwa mara ya kwanza nilikuta kunanguo na viatu vya kike nilipomuuliza akaniambia ni vitu vya yule girlfriend wake walioachana.. Akaniambia yule binti amesusa kuchukua hizo nguo na viatu kwasababu alinunuliwa na boyfriend wangu..
Kwa kipindi chote cha miezi mitatu tumeweza kukaa vizuri tu. Ki ukweli ananipa mapenzi ya dhati..Mimi ninakaa kwangu na yeye anakaa kwake so kila ijumaa mimi huamia kwake tunaspend wote weekend na juma3 asubuhi naamka kuelekea kazini na kuonana ni mpaka ijumaa tena.. Ki ukweli muda wote ninaokuwa nae sijawahi kuona wala kuhisi jambo lolote baya.
Ijumaa iliyopita nilipoteza pochi ikiwa na simu zangu zote na document za benki na vitu vingine vingi. Kwakuwa sikuwa na namna ya kuweza kutoa pesa, mpenzi wangu akanipa mwenyewe simu yake1 nitumie mpaka nitakapo kuwa sawa.. Tatizo limeanzia hapo wapenzi. Nilipofika kwangu jumatatu nimekuta mambo mengi kwenye simu ya boyfriend wangu hadi nashindwa kuamini..Mpenzi alisahau kulog out e-mail yake, akaunti yake ya facebook, twitter na hata kufuta sms za kawaida kwenye simu..
Nimekuta meseji za wasichana wengi kwenye simu wakiwasiliana na boyfriend wangu kwenye facebook, twitter,kwenye e-mail na hata kwa sms za kawaida wakimtaka kimapenzi... Ki ukweli wengi amekuwa hawajibu na wengine amekuwa akiwaeleza ukweli kuwa ana girlfriend. Kilichoniumiza ni kukuta dada aliyeniambia wameachana bado wanaendelea kuchart vizuri na huyo dada analalamika kwanini siku hizi anampotezea na anataka kurudi hapo nyumbani na boyfriend wangu anakuwa anamkatalia. Pia kuna mdada mwingine nae wamekuwa wanawasiliana na kupanga wakutane weekdays..
Roho inaniuma sana kwasababu nilikuwa nimempenda sana na bado roho yangu inampenda sana. Mpaka sasa sijamueleza lolote na nafikiria ijumaa hii nikikutana nae sijui kama nitaweza kuvumilia hasira zangu.
Naombeni mnishauri mdogo wenu nifanye nini..
Please Mange naomba usiweke e-mail address yangu hadharani.
Kuwasiliana na sisi tuma email kwenda
This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it