Who's Online
We have 383 guests online
EVENT YETU YA VALENTINE'S
Written by Mange   
Tuesday, 31 January 2012 23:29

 

Guys,

Nimefikiria nimeona kwamba ni bora siku hiyo ya shughuli tuende watu wachache, meaning tusizidi 50. Ili tusitumie pesa nyingi kwa ajili ya hiyo lunch ili tutumie pesa nyingi zaidi kutoa misaada.

Nimeona bora event iwe ya kawaida sana,tena sana, meaning kusiwe na makuu kabisa, ili msaada uwe mkubwa zaidi.

Wote tutakaokwenda tutavaa T-shirt za red, ambazo zimetolewa kama mchango na rafiki yangu kipenzi Joseline.

Tumetengeneza tshirt kwa size tofauti , small, medium & Large.

Kama ungependa kwenda kwenye hii event pls nitumie email humu This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it .


Jamani naomba wale waliotoa michango tu ndo wajitokeze kwenda. Sababu sidhani kama itakuwa na maana kama watakwenda wengi ambao hawakuchanga chochote nikawaacha waliochanga.


Pia nimeona tusiende na watoto wetu, sababu tukienda na watoto wetu tutakuwa busy zaidi na wanetu na sio wale watoto yatima ambapo sasa tutakuwa hatujafanya cha maana sababu point nzima ni kuwapa mapenzi wale watoto. Mie najijua Kenzo wangu nikienda nae sehemu ambayo hajui watu ananing’ang’ania nimbebe.

Event itakuwa siku ya jumapili Feb 12.



 

 

 

Comments
Add New Search
Anonymous   |2012-01-31 17:45:11
Safi sana bora umeweka kigezo hicho cha waliotoa michango ndio waende, nafasi
zikibaki anayetaka kwenda aje na mchango au atoe mchango maana wengine maneno
mengi wanasubiri wenzao wafanye wawe wadandie treni!

Lakini hata hiyo 50 bado
ni wengi ila waweza kufanya ndio maximum number. Na nyie mnywe soda tu huko na
biscuit watoto ndio muwapikie pilau na nyama. Wapate na juice basi watafurahi
sana, nina imagine kulivyo hata chakula kama hicho sidhani kama wanakipata.


Nimesuggest pilau kwa sababu kwa watu 200 unatumia mchele kilo 25, nyama kilo
12.5 na vitu vingine and doesnt cost much! Yaani kama ningekuwepo Bongo wallahi
hicho chakula cha watu 200 -250 ningewapikia kutoka nyumbani kwangu bure mkaja
kubeba tu mkaenda nacho. Lakini ndio hivyo bahati mbaya siko huko kwa sasa. Well
done Mange!
Suzie   |2012-01-31 18:10:48
Mimi nawahi nafasi ya yule dada aliyetuma western Union
Anonymous   |2012-01-31 18:28:23
shughuli mnazipenda na mkijua ni wabahili na wewe changa
japo kwa southern union basi kama western iko mbali nawe
Suzie   |2012-02-01 04:07:26
Usitushushue hivyo mwaya kuchanga tunataka uwezo balaa wengine ndo
tulishajizaliaga single maza plus vimshahara vya bongo, extended family uwiii
sijadaka umeishia kwenye bajeti. Vinguo nikileta mtasema nimechagua vilivyochoka
ila kwangu ndo mtoko wa wanangu. Ila sio issue tuko fit kwa maombi
Anonymous   |2012-01-31 19:02:03
Why can't you brown bagand not spend a dime out of the contributions?
kifimbo cheza   |2012-01-31 20:57:55
mshaanza ubaguzi,,,,, WALIOTOA wametoa kwa moyo mmoja!!! Sasa
unajuaje wengine walitoa mchango wa mawazo, wengine wanapanga kuja na michele au
nguo!! Hebu tutoleeni hayo mambo ya ubaguzi

kama idadi ipo weka idadi first
come first served ikitimia imetimia. Usiwanyanyapae watu kwasabu hawakutoa PESA.
Kwani wakija waliotoa michango peke yao ndo itakuwaje labda ninamiss a point
hapa, please nifahamisheni
Anonymous   |2012-02-01 06:22:17
Hata ukipeleka mchele bado unahesabika kuwa umetoa mchango, na haikusemwa kuwa
michango lazima pesa tu. Stop complaining!
Anonymous   |2012-02-01 02:54:10
Mange wanaoenda wanatakiwa wajilipie elfu kumi ya lunch sio waende tena
kupunguza share ya contribution!
Mange its not ethical to disclose health status
of that child with upele. The child deserves privacy, jamani wee ukipauka apo
tukasema umeathirika, how does it feel. Dont just say because they are kids, the
feelings are there,kama binadamu wengine. my 50 cents!
Anonymous1   |2012-02-01 03:09:55
mange naomba huyo mtoto aliyeathirika uhakikishe wamempeleka hospitali na
ameanza dozi,mbona ukimwi siku sio issue kama unatumia dawa ipasavyo watu
wanaishi mpaka miaka thelathini, huyo mtoto kwa muonekano tu wa utando
midomoni,upele anaonekana hatumii dawa,jamani kwa nini madaktari hawatembelei
hivyo vituo vya watoto ati.....pole sana mange kwa unayoyakuta na moyo wa
kujitoa japo jukumu hili ni la wote.
Anonymous   |2012-02-01 07:23:43
Mama mratibu, kwa vile kuna michango iliotoka uraya jamani! basi mimi
nitakuja katika tukio kwa niaba ya Joyce Midtgaard. Tshirt navaa Large
MINA   |2012-02-01 08:28:45
SAWA UMESOMEKA MAMA TUNAKUJA KABISA
kifimbo cheza   |2012-02-01 09:37:02
we anon 06.22.17 ukisoma vizuri nimesema pia how about ambao hawajachanga,
wanataka kuja na michele na nguo!!!!!
Nimekosea kusema PESA lakini
nilimaanisha michango kwa ujumla.
Harusi kwa kadi watu waliochanga na hata
mambo ya maana kama haya kwa watu waliochanga jamani. Hebu enlight me kwani
wakienda walichanga tu ndo inakuwaje??

Na pia kama waliochanga pesa au unga
nakadhalika wakizidi hamsini itakuwaje, itabidi waanza kuanagalia nani alitoa
zaidi ndo waje.

Inaitwa contructive criticizim, sio complain!!!!!
Lance Lowrey   |2012-02-01 09:52:47
Ufisadi Dot.com watu wametoa hela zao wewe unajifanya ooh shughuli mara
makuu..kwanini hukusema toka mwanzo kama ulitaka watu 50?? Mpare mpare
tu sio waaminifu hata kidogo..kuchakachua tu..Mpssxxyyyy
Anonymous   |2012-02-01 10:28:41
kumridhisha binadamu ni ngumu sana, nimeshangazwa na hii comment< mange
usipoteze muelekeo, cha muhimu ni kusaidia hao watoto. Wanaotaka kusaidia
watasaidia tu whether wapate nafasi ya kwenda ama la cuz eote lengo lao ni moja.
Sidhani kama kuna mtu atalalamika kakosa nafasi hata kama kachanga unless
alitaka kwenda kuuza sura.
Anonymous  - Eti loveness malinzi naye kaiga...   |2012-02-01 10:32:52
Baada ya kuona mange na hii idea...bibi dada naye kajifanya eti kuanzisha na
yeye harambee...watu wamekula buyu bora michango tulete huku jamani...kule yule
mwehu tu hana lolote anataka tu kula hela...
kifimbo cheza   |2012-02-01 14:15:13
wache waige tu HAKIHARIBIKI kitu kwani si mradi msaada unafika unapotakikana.
Its unfortunately sis wabongo we are not so creative sometimes hadi mtu afanye
kitu na mwingine aige. Na tena afanye mtu celebrity ndo wataiga,,, kwahiyo
usikonde mdau poa tu the more the merrier watoto waangaliwe ndo MUHIMU
Anonymous   |2012-02-01 14:18:45
Loveness Malinzi ndo nani jama?
Anonymous   |2012-02-01 10:34:06
jamani kweni mmetoa michango ili mkaile wenyewe au kusaidia hao watoto
mbona mwalilia kwenda hahahaa
Anonymous   |2012-02-01 14:19:34
Tunataka kwenda kuwa na watoto na wala sio kula au kunywa, sio kwamba tunalilia,
tunataka kujumuika nao jamani
Anonymous   |2012-02-01 10:38:04
Watu bwana Kwani lazima muwepo wote hivi hamuwezi kuchangia na kuendelea na
ratiba zenu imekua harusi lazima wote mfike duuh it's just charity sio lazima
watu wote wafike,
Anonymous   |2012-02-01 14:16:49
Najua hapa sio mahala pake wana uturn mtanisamehe lakini naona bora niseme nitoe
duku duku langu, mkiweka madole mekundu, ya blue kijani I dont mind.

Ila
ninachouliza ni hivi, hivi jamani inakuwaje mwanaume mzima unaacha shughuli zako
unacopy na kupaste nyumba ya mtoto mwanamke kisha unaisambaza dunia nzima kwa
email huoni aibu? Mbona huo ni ushamba uliopitiliza, huwezi kuona kitu kwa macho
ukaapreciate kisha ukaendelea na maisha yako?

Na nyie mnaoforwardiana kwa
email mmekosa kazi ya kufanya? Au ni wivu au ujinga? Mbona majuu nyumba za
macelebrity zinatolewa mpaka kwenye magazeti lakini huoni wazungu wakaacha
shughuli zao wakawa wanatumiana hiyo picha za nyumba kwenye maemail? Jamani
Ubongo au UTZ kweli mzigo, mimi aliyeniforwadia nimedelete, ndio nyumba nzuri
sana, what for? Get a life fanyeni kazi mtafute pesa mjenge zenu.

Mwammy
kwanini usimshtaki huyo anaesambaza hiyo property yako kwa email? You can start
at th...
Anonymous  - Wanawake wa bongo   |2012-02-01 14:51:22
Yaani wanawake wa bongo mmejaliwa midomo sijui hata hizo chapati
mwazikunjiani.Midomo juu juu saa sote.
Kila Mange asemacho lazima kiwe
criticized its a courtesy yeye kusema what she thinks asiposema kosa akisema
kosa .Mwacheni mtoto wa mwanamke mwenzenu.
Hapo Mange amechakachua nini na
wewe?usituletee mambo ya ukabila hapa.Toa boriti jichoni kwako kabla ya la
Mange.
Ubinadamu kazi sana ndio maana hata maendeleo hayapatikani maana ni
midomo tu .
Anonymous   |2012-02-01 15:28:55
Anonymous wrote:
Baada ya kuona mange na hii idea...bibi dada naye kajifanya eti kuanzisha
na yeye harambee...watu wamekula buyu bora michango tulete
huku jamani...kule yule mwehu tu hana lolote anataka tu kula hela...
jamani bahati ya Mange usilalie mlango wazi...Mange mtu wa watu..yule
malaya ni mtu wa nani?!! Maringo kibao...my dad house sijui
nini?!! Jamani kaiona mwamy's mansion?!!!
Anonymous   |2012-02-01 15:52:22
nimecheka jamani wana u-turn mnavichaa sasa hao wanaotaka kwenda kwa niaba ya wa
ulaya au wa westen union INAHUU?
Anonymous   |2012-02-01 16:51:42
Mange i suggest only few representatives should go may be like 5 to 10 people
minimum coz this is about the children not the people who contribute the money
the focus should be on them kids and the kids only 50 people is too many.Tena it
would have been even better you pick 10 people ambao hawakua na uwezo wa
kucontribute nothing to go with you that way kwenda kwao ndiyo contribution
yao.CONTRIBUTION IS NOT ONLY MONEY IS YOUR PRESENCE AS WELL!!! im just
saying

shosti from ATL....
matem   |2012-02-02 05:30:08
kweli kabisa mange msiende 50 chagua watu 10 tu,watotot 117,muende 50,no
way,tafadhali watuwakilisheee.
matem   |2012-02-02 05:32:42
mange your great kwa sababu you have a thickest skin,manake mishushuo ya humu
ndani ni balaa,go mange mwaya.unathubutu kwa kweli na MUNGU akuzidishie
:
matem   |2012-02-02 07:28:23
kungekuwepo pia na ofisi nyingine ya kuleta misaada maeneo ya posta,wengi tupo
huku pia na hatuna usafiri,utoke job saa kumi uje mpaka huko inakuwa ngumu kwa
kweli
JL   |2012-02-02 08:14:18
Mange uko sawa bana sio lazima muenda woteeeee
au wengine mnataka mtokee
u-turn?

Pia vizuri kuwaacha watoto wenu majumbani kwani mtaenda kuwa nao bize
kule halafu mtazidi kuwasononesha watoto wa kituoni, watatamani nao wazazi wao
wangekuwepo
Anonymous   |2012-02-02 08:19:27
nawe uliyekuja na story za nyumba ya mwamy una njaa wewe unajipendekeza tu kwani
nani kaulizia nyumba ya mwamy hapa! wewe vp? tena wewe ndo mwenye wivu
unajishaua hapa eti ulitumiwa ukafuta! uliifuta kwanini sasa kama siyo wivu
anayeisambaza sio kwamba anamwonea wivu anawapa watu changamoto za maisha wajue
fainal uzeeni!! siyo kujirusha tu. nyoooooooooo
Anonymous   |2012-02-02 18:36:20
Wee hayawani na tena hamnazo, na inawezekana wewe ndio uliyecopy na kwenda
kusambaza huko kwenye mitandao kwa ushamba. Isitoshe kwani huwezi kuwa inspired
kwa kuona tu? Mbona majumba yamejaa tele Masaki, Mbezi beach na Bahari beach
ukitaka kuwa inspired si ufunge safari ukaone. Isitoshe hujui katika hao
unaowafordia watakuwa inspired kujenga au kwenda kumdhuru, hujui nani mzuri wake
na nani mbaya wake.

Sio wewe tu wote wanaokazana kuforwad nyumba ya mwana wa
mwenzenu acheni huo ushamba mzigo, mngekuwa nje ya nchi mngechukuliwa hatua
nyambaff. Ningekuwa mimi pia nisingependa mahali ninapoishi na mwanangu pawe
exposed dunia nzima, mumfikirie yule mtoto wake wakitokea vichaa wakaamua
kufanya la kufanya? Utakuja hapa kutukana? Use your brain, she need privacy
because she need to protect her child. On the other side hata wewe ukitaka
waweza kukopa ukapata nyumba kama ile, mdogo wangu ana duka Kariakoo kanunuliwa
na Bank yakwake...
Write comment
Name:
Email:
 
Website:
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
:confused:8):lol::x:P:oops::cry::evil::twisted::roll::wink::!:
:?::idea::arrow::blink::dead::coffee::karate::gossip::hahaha::newpost::love::lips:
:no::nono::rofl::shrug::stop::tape::thumbsup::wail::waves::yahoo::yes:
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

 
 
Follow Mange on Twitter
Find U turn Blog on facebook