Who's Online
We have 381 guests online
KUELEKEA EVENT YETU YA VALENTINE'S DAY.....
Written by Mange   
Tuesday, 31 January 2012 21:21

Leo nilienda tena Kurasini National orphanage centre.

Lengo langu leo lilikuwa ni kuongea na management ili tupange vizuri

mlolongo mzima wa event.

Alhamdulillah, everything went well...

 

Then nikaenda kuwaona wale watoto wadogo, wakubwa bado

walikuwa shule...

this is them taking their afternoon nap...

yes ,they nap kwenye mkeka....sakafu inavyoumiza sasa

ila usiku wanalala kwenye dorm zao...

 

 

Chatting with the kids...i love this little girl...she is super cute, her name is

Asha, jina la marehemu mama yangu hilo....

 

 

Hanging out with the kids...

 

nilijairbu kuuliza kwanini watoto wanatembea bila viatu au hata

kandambili. nikaambiwa wamepoteza...

sasa wakikanyaga miba inakuwaje jamani...

one of the things i plan to buy ni kandambili....

 

Also i asked kwanini watoto ni wachafu, nguo ni chafu,

nkaambiwa hawana nguo za kutosha,

so kwa wale ambao hamna uwezo wa kutuchangia cash

tafadhali kama una nguo za watoto used naomba unipe....

 

nikiwa na watoto wachache kati ya watoto 117 wanaolelewa hapa...

wengine ni wakubwa zaidi niliambiwa bado wapo shule...

 

 

they are such happy souls....

 

Huyu binti alinisikitisha jinsi alivyoharibika ngozi....

 

 

ngozi ya mtoto...

 

Nikimuonyesha mlezi wao jinsi mtoto alivyoharibika ngozi

na nikimuuliza wanampaka dawa gani, au kama keshafika kwa daktari.

nikajibiwa mtoto ni mwathirika wa HIV.

nikamwambia hilo sio jibu dada hata kama ni mwathirika,

still anatakiwa awe anatumia dawa kwa ajili ya hii.....

i felt really bad....

 

Nikicheka na watoto....

 

last time nilivyokwenda wakati naondoka niliwaambia watoto nawanunulia soda

na biskuti ,basi nikamwachia kaka mmoja pesa,huyo kaka ndo alienipokea siku hiyo.

basi na leo wakati naondoka nikawaambia tena watoto nitawanunua soda na biscuit,

kitoto kimoja kina kama miaka 5 hivi kilinishushuaje sasa,

akasema, we dada miyeyusho, hata mara ya mwisho ulisema utatununulia soda hukununua

uwiiii, kabla sijajibu nilianza kucheka kwamba,

try to imagine katoto kadogo kanasema neno 'miyeyusho'

vitoto vina maneno hivi...

DUh ,i felt really bad kwa kweli, so nikawauliza wote kwa pamoja

mara ya mwisho nilivyoondoka hamkupewa soda au juice au biskuit

wakasema hapana hawakupewa.

i was just like DUH...

So, nikasema leo siondoki hadi nivione vimeletwa

 

nilikalishwa 1hr eti juice na biscuit zimefatwa dukani.

ila nilikaaaaaa, hadi vikaletwa nikawaacha wanakula ndo nikasepa zangu.

kwa kweli im disappointed jamani, sijui cha kufanya na nchi hii.

sijui ni huu umaskini umezidi hadi mtu anaweza kuwacheat watoto kama hawa

hela ndogo tu ya soda na biskuti???

Ila lesson learnt, hakuna kuacha cash, hata iweje,

 

 

Nikimfungulia mtoto juice...

yani kwetu sie juice na biscuit ni kitu kidogo sana, ila ungeona jinsi watoto

walivyoruka ruka baada ya kuona juice na jinsi walivyoniambia ahsante.

 

 

 

 

HOW DO WE CHANGE THINGS IN THIS COUNTRY???

 

HOW DO WE MAKE SURE MISAADA INAWAFIKIA WALENGWA???

 

 

Naomba muendelee kuchanga

Western union : Mange Kimambi Lowrey – Tanzania

MPESA: 0769 781315

 

Comments
Add New Search
Anonymous   |2012-01-31 16:21:08
Jamani huyo mtoto mwenye HIV, sasa mbona wanamuweka tu na hawa wengine, vituo
vingine wakishakuta ana HIV wanawapeleka kwenye vituo vyao maalumu.Sasa jamani
hiyo ngozi, hemu mnaofahamu tusaidiane mawazo, MAFUTA GANI ATUMIE, kwenye hiyo
siku tujitolee wengine tumletee hayo mafuta na wakiyaiba wakapake wao MWENYEZI
MUNGU ATAWAADHIBU, KAMA HUYO KAKA ALIYEKULA HELA YA SODA YA WATOTO JAMANI,
anafikiri hiyo hela atanunulia gari?.Dunia hii jamani, ndio tuna shida lakini
hela ya watoto yatima ya soda nayo tunatia ndani???
Mungu amrehemu mamako
Asha,apumzike kwa amani,ndio mana mungu amekukutanisha na huyu Asha
mdogo.
Watoto wanatia imani sana, nikiangalia watoto wetu walivyojaza matoy
ndani na wanalala pazuri nasema eeh mwenyezi mungu wasaidie hawa watoto.Tutakuja
Mange.Ila idea ni bado vilevile kuwa tuje na watoto wetu wacheze hapo au tuje
wenyewe?????
Anonymous   |2012-01-31 17:23:28
Kwa hiyo kama mtoto wa ndugu yako ana HIV hataishi pamoja na wanao utampeleka
sehemu maalumu?

Mimi ninalea mtoto wa marehemu ndugu yangu ni HIV positive na
tunaishi nae nyumba moja na tunamtreat sawa na watoto wengine. Kutokana na
mawazo kama yako ya kuwatenga watoto, huyu mtoto wangu kipenzi ambaye
ameathirika walikataa kumpokea shuleni kisha tulielezea status yake. Wenziwe
wakaanza shule yeye akabaki nyumbani ingawa ana bidii ya kusoma. Jamani tuache
hii tabia ya kubagua watoto kwa kuwa tu wana virusi, hawaambukizi kwa kuwashika,
kukaa nao au kula nao chakula pamoja. Duh na watu wamekuunga mkono kabisa!!
Anonymous   |2012-01-31 18:26:24
JAMANI WADAU NAONA SIJAELEWEKA VIZURI, SIJAAMAANISHA WENYE HIV WATENGE ILA
NASEMA KUTOKANA NA EXPERIENCE NILIYOPATA KWA KUHUSIKA NA COMMUNITY WORK,
TUMETEMBELEA SANA ORPHANAGE CENTRES MIKOANI. SABABU WATOTO WAKO WENGI, HAWAPATI
ATTENTION YA KUTOSHA JINSI WANAVYOHITAJI, SO UNAKUTA WENYE HIV MARA NYINGI
WANAPELEKWA VITUO VINGINE WAHUDUMIWE HUKO, KUPUNGUZA KASI YA KUAMBUKIZANA NA PIA
WAPATE SPECIAL CARE.MTOTO WAKO AU WANDUGU UNAYEMLEA NYUMBANI NI TOFAUTI, UNAMPA
ATTENTION YA KUTOSHA, SASA HUKO VITUONI MFANO AKIWA NA VIDONDA KUZUIA WATOTO
WENZIE WASIVIGUSE OR SO KATIKA SEHEMU KAMA HIYO NI NGUMU SANA,NDIO MANA
NIKAULIZA HAPO JUU.SIWEZI KUNYANYAPAA MTU WA HIV HATA SIKUMOJA MANA LEO KWA
MWENZANGU KESHO KWANGU.NATUMAINI NIMEELEWEKA.
Anonymous   |2012-02-01 13:27:23
SIO UBAGUZI NDUGU. WATOTO UKIWAACHA WACHEZE PEKE YAO WANAWEZA HATA WAKAMSAIDI
KUMKUNA HUO UPELE NOT KNOWNG THE EFFECTS. UNLESS KILA MTOTO ANA MLEZI . WA
NYUMBANI KWAKO UTAMTREAT THE SAME BUT AM SURE HUTARUHUSU ASHEE KIKOMBE AU KIJIKO
NA WA KWAKO AMBAYE NI MZIMA, BISHA!
Anonymous   |2012-02-01 13:49:13
Umemshambulia mwenzio kuhusu sijui kuwatenga watoto, haya, na wewe what have u
done baada ya mtoto kuambiwa hawezi kuingia hiyo shule? umemtafutia nyingine au
kisa sio mtoto wako ndo maana "wenziwe wakaanza shule na yeye akabaki
nyumbani...." nimekunukuu wala usinibwatukie, ni maneno yako, labda
uyakanushe au kuya re-phrase.
Anonymous   |2012-01-31 17:46:28
katika familia yenu akitokea mtoto ana HIV mnampeleka kuishi vituo maalumu au
atakaa na nyie hapo nyumbani???......watu huwa mnaongea tu coz sijui hamjawahi
kuishi na wenye HIV.....huu ni ugonjwa ndio but it doesnt mean hastahili
kujichanganya na watu....na ukute hao wanaoonekana wazima nao wanao sema dalili
hazijajitokeza....unyanyapaaji hautakaa uishe kamwe kwa kauli na mawazo kama
haya!
Anonymous   |2012-01-31 18:30:56
Nyie ma anon wawili hapo juu mbona hamjamuelewa mtoa mada wa kwanza, yeye
hajasema kuwabagua wenye HIV kasema tu kuwa huwa wanawekwaga sehemu tofuti, YES
hata mimi najua hivyo, nishasikiaga wanapimwaga mara 3 wakishaconfirm wanao kuna
vituo flaniflani huwa wanawakusanya wanawaweka, tena kimoja kiko
Dodoma.Msilinganishe malezi ya vituoni humo na malezi mazuri mnayotoa nyie
majumbani.
Huyo binti ni utangotango huo au sijui tuseme mba, tumtafutie dawa
tupeleke.Atapona.She is so innocent.
DESPERATE HOUSE WIFE   |2012-02-01 12:20:02
MI PIA NIMEMUELEWA MDAU WA KWANZA HAPO JUU. NA PIA NA SUPPORT IDEA YAKE. HUYU
MOTOTO AMEPEKWE SEHEMU AMBAYO WATAMTUNZA ZAIDI KUTOKANA NA UGONJWA WAKE. MFANO
MZURI MKIANGALIA HAPO ANAVIDONDA HIVO MWILINI NA KWANI WAMEMSAIDIAJE? WANABAKI
TU KUSEMA ANA UKIMWI. ANGEKUWA KITUO MAALUM CHA WATOTO WAADHIRIKA WANGESHATAKE
CARE YA TATIZO LAKE MAANA NDIYO KAZI YAO NA IM SURE WATAMPA ATTENTION ZAIDI.
HAPO ALIPO NAFIKIRI ANAKUWA TREATED KAMA HAO WENGINE AMBAO NI WAZIMA. SHE NEEDS
EXTRA SPECIAL CARE. MIMI NDO NILIVYO MUELEWA. THIS IS A GOOD JOB MANGE,
UBARIKIWE WEWE NA WENGINE WOTE WALIO JITOA. MUNGU HUWABARIKI ZAIDI WANAO BARIKI
WENZAO. NAFIKIRI KATIKA BUDGET YENU MUMTENGEE HUYO MTOTO EITHER AENDE KUMUONA
DACTARI WA NGOZI AU MUMTAFUTIE DAWA WENYEWE. NA HELA MJUE KABISAA ZIMETUMIKA
KWAAJILI YA HAO WATOTO. I IMAGINE KWAMBA HIVI VITUO VINAPATAGA MISAADA YA HAPA
NA PALE LAKINI ONLY GOD KNOWS HOW MUCH GOES TO HELP THOSE KIDS. SHAME ON THEM
A...
Anonymous   |2012-01-31 17:49:04
AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE ILA NAONA MWENZETU UNA WE UPARA!
koku   |2012-01-31 16:24:47
hadi hapo nadhani umeshapata jibu mange. hakuna kuwapa CASH hao walezi wao.
ni bora kila kitu kinunuliwe na kionyeshwe mbele ya watoto,na
kama kutakuwa na vifaa vilivyonunuliwa basi kuwe na follow
up,otherwise hata hizo kandambili watawanyang'anya hao yatima na
kuwapelekea watoto wao majumbani. inasikitisha na inakatisha tamaa  
na walaaniwe wale wote wanaowadhurumu yatima  
Anonymous   |2012-02-01 04:30:05
NA WEWE UMETOA MCHANGO KIASI ANI ?AU KUTOA MAELEKEZO TU KWA PESA ZISIZOKUHUSU?
DESPERATE HOUSE WIFE   |2012-02-01 12:22:17
ATA KAMA HAJATOA LAKINI MAWAZO NAYO NI MCHANGO NA UNAJUAJE HAJATOA? CHANGIA CHA
MAANA KWENYE HII TOPIC NA SIYO KUANZA KUTOLEANA MANENO YASIYO NA MAANA. TUSUBIRI
TOPIC ZA UDAKU TUKAGOMBANENI HUKO LAKINI KAMA HII, SHOW RESPECT PLZ
Anonymous   |2012-02-01 13:29:30
ADVICES NI MCHANGO VILE VILE. KWANI MA-FINANCIAL ADVISORS PESA HUWA ZINAWAHUSU?
Anonymous   |2012-02-01 13:52:17
Was just wondering, kama michango ikifikia milioni 20, tutanunua nguo, toys na
chakula tu au? au tutakuwa na "standing order" ya kununua hivyo vyitu
montly mpaka pesa ziishe?
Tufikirie na vitu vikubwa vya kufanya kama hela
itatosha mfano kujenga choo cha kisasa au kununua more vitanda ili watoto
wasishee kitanda kimoja watoto wa4 etc
kiche   |2012-01-31 16:25:46
kwanza nakufagilia sana kwa kwenda kuwaona hao watoto mungu akubariki.ukienda
next time hizo biskut na juice toka nazo huko unakotoka uwapelekee mwenyewe
mkonon.

mimi nataka kutoa msaada ila naomba jina la kituo na ni nini
wanachohitaji natuma mtu apeleke msaada wangu.

Sister mange wabongo wana maneno
sasa usitake hizo hela ziingizwe kweye account yako watu hawatakuamini
kifimbo cheza   |2012-01-31 16:31:58
du shame on him kaenda kula hata pesa ya soda jamani!!! Kumbe unaacha pesa
inasaidia mi huwa naona kinyume sana. Mana umesema ndo mana huyo mtoto akajibu
lasivyo ingeishia huko huko na hii ya leo pia ingemezwa

I really hope huyo
mtoto anapewa dawa hata antiviral za HIV mana jibu la huyo dada haliridhishi
kabisa!!!! Eti kaathirika kwahiyo.


Kila sehemu kuna utata uaminifu wa pesa,
lakini nchi yetu imezidi sana. Na pia uaminifu wa hadi wa mapenzi ya ukweli
tizama tunateketeza watoto namna hii, kama mimi na wewe tukajiheshimu basi walau
tutapunguza watoto kupata magonjwa kupitia kwetu.

eeh mwenyezi mungu,
tunakushukuru kwa kila jambo na kwako tunakuomba, utupunguzie mitihani hii
watoto wetu uwatizame. Mwenyezi mungu awape nguvu na imani hao watoto na
wahusika wote wenye nia njema nao.
Anonymous   |2012-01-31 18:33:57
yes, mimi pia i hope huyo mtoto mgonjwa anapata dawa, ndo maana mdau mmoja hapo
juu kasema anashangaa whu yuko hapo, huwa wanawekwaga sehemu zao zingine huko
wanapewa huduma special.mtu kasema hapo badala ya kukaa mfikirie mnakuja juu
kusema ananyanyapaa wagonjwa wa HIV.
Its true mdau wa hapo juu kabisa, huwa wana
vituo vyao maalumu wanakusanywa na kupata huduma nzuri zaidi huko, tatizo vituo
havina ushirikiano wa kutosha so wengine hawajui au wengine watoto zao
hawapokelewi.Wakatoliki wana system yao nzuri, vituo vyao watoto wenye HIV
wanachukuliwa wanapelekwa sehemu moja.
Anonymous   |2012-01-31 16:43:05
mange hongera sana kwa unayoyafanya.upo juu kama jumba la mwammy.hata sijui
niseme nini kwa kweli.inaonyesha katika misaada inayotolewa,ni asilimia chache
huwafikia walengwa.kwa nini lakini?jee ni nani wa kulaumiwa?maana kuanzia ngazi
za juu,hao mafisadi nao wanakula kwa upande wao.na
ungeondoka,visingenunuliwa.wewe saidia fungu lako utalipwa na mungu.maskini kwa
huyo mtoto mwenye matatizo ya ngozi.
superbig   |2012-01-31 16:50:36
thank you so much mange for showing us the way.....Mungu akubariki
sana.
Honestlly i have learnt alot from you...kujali na kutoa kwa moyo
wote..... please dont giveup nomatter what n always God will be there for
u.......

BIG UP GAL
anonymous  - Ngozi ya mtoto   |2012-01-31 16:51:58
Huyo mtoto jamani ni mba.Due to Poor hygiene,Poor immune system,Chronic illness
and others .The best shampoo choices include antifungal shampoos such as
ketoconazole (Nizoral).

Mtakaoenda u can get that shampoo and a cream to apply
every day ad in a couple of weeks she will be fine.Tatizo hao walezi hawana wito
so na hivyo vitu si ajabu wakavibeba na kupeleka makwao.

I think Mange if u
will be in bongo after a week of event nenda tena ukaongee na hao watoto they
will tell you lots.kama hawakupewa vitu au walinyang'anywa watakuambia tu.

When
i think of bongo i tear.Most people are so deep pocketed but short armed.
Anonymous   |2012-01-31 17:19:33
Jamani mpaka machozi yamenitoka, watoto wanatia imani. Jamani mlio nje ya nchi
hasa UK mnaweza kununua toys kwenye charity shops au hata kwenye carboots. Mimi
mission yangu kuanzia leo ni kuwapa hao watoto furaha na matumaini, nitakuwa
ninaenda kwenye charity shops na carboots kukusanya toys na nguo maana huko
unapata hata kwa 20pence. Nitakaporudi nyumbani Inshallah nitakuwa nimefungasha
furushi la nguo na toys kwa ajili ya hao watoto.

Na njia nyingine ni kupata
mtu wa kutengeza Murals kwenye hizo sehemu zao. Mange nitawasiliana na wewe
uniulizie kama nitakubaliwa si unajua tena za kibongo kibongo unaweza ambiwa
marufuku kuchora chora humu! The place is so dull wala haionyeshi kama inaishi
watoto. Mungu turehemu!
Anonymous   |2012-01-31 17:55:36
una machozi ya karibu kweli yaani umelia kwa hizi picha tu au umekumbuka
mengine?......tanzania watu wana shida sana magonjwa kibao, walemavu ndio
usiseme wana hali ngumu sana, bado yatima kama hawa.....watanzania wote tunajua
nchi yetu inamatatizo but huwa hatuko mstari wa mbele kusaidia wenzetu hata
kuwakumbuka tu kwa sala mpaka mmoja aamue kuonyesha njia ndio machozi yanatutoka
mmmh!.....Mungu tunusuru!
Anonymous   |2012-01-31 21:53:12
Labda wewe una roho ngumu, mimi siwezi kustahamili kuona watoto wadogo au watu
wakipata tabu kama hivyo hata kama ni nchi nzima. Pili usifikiri kuwa watu wote
huwa tunatangaza tunayoyafanya au haya mambo tumeyajulia au kuyaona kwa Mange.
Tangu mwaka 97 nimekuwa nikilia na nitaendelea kulia kwa sababu emotionally tuko
tofauti.

Labda kwa kifupi tu maisha yangu yote nimekuwa nikijitolea, ninalea
watoto yatima nyumbani sasa hivi ambao ni wadogo, wengine niliolea wako wakubwa
wameshaoa na kuolewa; baki ambao wamebaki na mzazi mmoja ninaowasaidia ada na
mambo mengine. Sina utajiri wowote mshahara wangu tu ndio unaofanya hayo. Na
mbali ninaowajua hata nisowajua pia nimewasaidia. Kwa kuwa nimeweka anonymous
hakuna mtu anayejua jina, kutokana na kazi yangu nimejenga madarasa, zahanati,
labour rooms, na mabweni ya kulala watoto wa kike na wa kiume kwa miaka kibao
mpaka nilipoacha kazi. Achilia mbali watoto waliolipiwa ada za shule na hi...
Anonymous   |2012-02-02 10:54:31
hongera dada, Mungu na akuzidishie,ila kwa sk ingine usipate shida ya kujieleza
kwa juha kama huyu
Anonymous   |2012-02-01 13:32:05
WENGINE SIYE MACHOZI YETU YAKO KARIBU KAMA YA KIM KARDASHIAN....THAT BITCH CAN
CRY!
Anonymous   |2012-01-31 17:30:24
I hate those benches they remind me of government hospital like Temeke and Mnazi
mmoja! Why they put them for kids, I have no idea! Sasa hapo watoto wanakaa
matako yote yanauma, anyway watu wanashindwa kuwa hata creative, room ya kukaa
watoto wakapumzika iko kama hospitali, mabenchi kama wafungwa, Jamani Uyatima
mbaya nyie acheni tu.

Mungu naomba nijaalie niweze kufanya jambo la
kurekebisha hiyo sehemu wanayopumzikia hao watoto at least iwe room ambayo
itawapa matumaini, room ambayo yenye muenakano wa kuwa sehemu ya watoto ya
kucheza na kurelax.

Mange mkiweza kupata magodoro yale madogo yale chini ya
single size (maana size hiyo hawawezi kupeleka makwao) kama ya baby cot yazidi
kidogo tu waweza kununua japo hata 5 au 6 kwa kuanzia ili hao watoto wasilale
chini!
Anonymous   |2012-01-31 17:45:02
mange naona unasafisha njia kabla ya kuingia politics za bongo- good move
mistress ya obama   |2012-02-01 06:58:10
na nyie jamani mtu akiwa na wazo zuri la kusaidia mnaingiza mambo ya siasa
ndani, ina maana watu wote wanaosaidia mayatima au kuwasaidia wasio na uwezo wa
kupata elimu na wao wanataka kujiingiza kwenye siasa? mie naona siasa za bongo
zimewaathiri kisaikojia saa ingine jaribuni kuwa na utu, ni hayo tu!
Anonymous   |2012-01-31 17:55:29
Mi bado nalia na Mange kuwa na registered organisation sio mambo ya kuomba hela
iwekwe kwenye account yake.. accountability wapi mama? Utafungwa siku moja.
MANGE lowrey   |2012-01-31 18:03:07
kama ingekuwa ni long term plan yes ningefanya hivyo but for now its just an
event, nikafungue an NGO sababu ya event moja?

na kwa taarifa yako pesa hazina
usalama wowote hata kama zingeingia kwenye account ya foundation still mimi ndo
ningekuwa signatory na ningeweza kufanya chochote kile na hizo pesa. cha maana
ni uaminifu tu. i will post an excel sheet na michango yote FEB 1OTH. na pia
ntaweka mahesabu yote ya kuwa pesa zenu zilitumikaje.

kwa jinsi ulivyo na mdomo
mrefu my guess is Hujatoa hata senti moja ya mchango...lol

MANGE
new version   |2012-01-31 18:20:47
weee Mange weee chapwa wewe...mama, the only change for TZ will come
through prayer and system overhaul...whats happening at the bottom is what
trickled down from the top
Anonymous   |2012-01-31 21:33:06
Kutoa ni moyo kila mtu anahaki ya kuuliza maana ubinadamu kazi sana.
Umetuonyesha yote kuhusu watoto yatima tunashukuru. Swali ni kwamba ndugu zako
wote wanauwezo wa kutosha, mpaka umetoka kwenda kusaidia wengine mwenyezi Mungu
hapendi watu wanaojifanya wema kumbe yanayowahusu sana wameyaficha.
Anonymous   |2012-02-01 06:27:48
Hao ndugu zake ni yatima? Walemavu wasioweza kufanya kazi? After all Mange
amefanya mobilization na watu wametoa michango ili kusaidia watoto yatima na si
ndugu zake.

Usikute wewe ndio design ya kula misaada ya watu kwa kisingizio
cha kujisaidia na kusaidia nduguzo.
Anonymous   |2012-02-01 07:13:49
wee habari ya ndugu iache kabisaaa, tuna wasaidia sana shukrani yao ni bure
kabisa na bado hujapigwa vibomu ambavyo wala havina umuhimu zaidi ya kukomoana,
saa nyingne ni bora kuwasaidia hawa yatima wakifurahi unapata thawabu mara mia
kuliko ndugu wasio na shukurani!!
JUDITH   |2012-02-01 09:50:08
MANGE NA WEWE UNAMJIBU WA NINI HUYO FALA ANADHANI NA WEWE UNASHIDA YA MBOGA KAMA
YEYE,,,USHAZOEA KUTAPELIWA NA WANAUME UNADHANI MANGE NAYE TAPELI KAMA MABASHA
ZAKO WANAOKUFIRIKISA UCHOCHORONI???UTAKPPWA MPAKA UANZEISHE ORGANITION YA MKND
FALA WE
bakari   |2012-01-31 18:16:55
your doing very good job! keep it up.
Anonymous   |2012-01-31 18:33:56
KUIBADILISHA NCHI JINSI ULIVYOULIZA ....NI KUBADILISHA CHAMA KINACHOTAWALA TANGU
AWALI ZA MABIBI NA MABABU ZETU. WE NEED CHANGE!
hannah   |2012-01-31 18:42:19
hahahahahah,mange umenichekesha sana,ni kweli pesa hazina usalama wowote,cha
muhim ni uaminifu wa mtu baaasi..Mungu akubarike mama!!
Anonymous   |2012-01-31 18:58:35
mnge vipi maadui zako wanawezaje kuchangia anonymously? yupo mmoja anataka
kukutumia hela ila ataki ujue ni yeye. ameguswa na hii project. weka majibu humu
humu
Parrot   |2012-02-01 02:23:21
nenda kituo chochote cha Mpesa ukamtumie. Kama uko nje ya tanzania fanya
kumtumia ndugu au jamaa unaemuamini kisha umwambie amtumie mange
kwa mpesa. Ila hutojua kama zimefika au la maana hawatoi risiti, labda
aimunch ile screen kuonyesha kiasi gani kimetumwa kwa muhusika
kisha akuonyeshe.

Njia nyingine ni kumtuma mtu ampigie mange
wakutane amkabidhi kisha akupigie simu uongee na mange aconfirm kama kweli
kapokea.
Anonymous   |2012-02-01 07:15:05
mwambie achangie tu hela sio ya mange!
Mama D   |2012-01-31 19:15:15
Mungu awe nawe na hao malaika. Mungu atazame roho za wahudumu na kuwaondoa mzizi
tamaa, Mungu aitoe adhabu ya ukimwi kwa watoto, Mungu abariki mikono yote
iliyotoa chochote, Mungu awavishe haya wezi wa Mali za yatima, Mungu atujalie
uaminifu katika ndoa zetu, Mungu anisaidie niweze fungua kituo cha yatima
wenzangu kwani uzito wa mzigo ni kwa aliyeubeba. Mungu awabariki watanzania na
nchi yetu.
baby ya Mange   |2012-01-31 19:34:18
this is real man!! ...sure God is working with u my love and we r all
blessed through u Mange...my thought and prayers goes out to all orphans iin the
world...may God bless them.
baby ya Mange   |2012-01-31 19:44:27
baby why dont u go see optician kama macho yanakusumbua??may be they will
prescribe u wit normal glasses..or give u medicine or any ointment....
baby ya Mange   |2012-01-31 19:45:54
u looking good baby! nimependa top ilivyokukaa hapo kifuani...
romiego   |2012-01-31 19:49:56
mange umechoka hebu jiangalie tena yan kama umetoka kuchezea dudu kabla hujaenda
kwenye hiyo orphanage yan umechoooooooka na kulegea
Anonymous   |2012-01-31 20:32:30
Halafu why one time event you have the potential to make it long term ndio maana
yake. You can work from any corner of the world kama una wanachama TZ.

Nachanga
sana kwa njia ambazo sina haja ya kueleza hapa. Kwako nangoja nione
utakavyotumia ndio unihamasishe.

Usiwe mwepesi kujitetea ukipewa mawazo
endelevu. Ukisifiwa ulivyopendeza nguo ndio unaona raha, pokea pia hoja za nguvu
na mikwara ujiboreshe.

Hao hao mashoga wanaotuma kwa WU watakugeuka, usione
sasa wako diplomatic wanakupa moyo, subiri kizaa zaa ukichezea hela ya mbeba
mabox.

Bye!
kifimbo cheza   |2012-01-31 20:48:52
zinaitwa COMMUNITY DEVELOPMENT work, kazi zinafanywa through negotiation
(bottom-up) approach. Through hizi community development ndo tunaweza kuLOBBY
policies hata kwene existing government.
Sio tu kung'ang'ania tu ubadili chama
halafu ndo iweje wakija hao chama kingine na mambo hayo hayo. Hizi community
work ziko in high rise mahala kwingi, na inshAllah iko siku tutafika tu (i mean
kwenye aim ya change tunayoitaka) na ku ensure SUSTAINABLE development.

by
the way, nilichapia hapo juu, nilimaanisha KUSEMA kama unawaachia watu pesa
KUNASAIDIA saa nyingine
Anonymous  - UTANGO UTANGO   |2012-01-31 20:52:48
Hivi utango utango unaitwaje kiEnglish, tukijua tunaweza ulizia uzuri. Wengine
hatujui hata tukitaka ulizia dawa chemist hatutojua tunasemaje
Anonymous   |2012-01-31 21:06:02
ka jamani yaani hawana hata toy hata basi vijigari na mabembea ya uongo uongo
mange mimi niko mbali natamani hawa watoto wapate toys mange please huo mchango
wenu wanu nulieni hata toys za kuchezea mfano midoli,vitabu,magari,please jamani
tuwasaidie mimi nafanya mpango nikusanye toys kwa wenzangu huku uk zikikamilika
mange ntatafuta jinsi gani zitumwe bongo ,ntaomba msaada wako wa kuzitoa
bandarini na kuzipeleka.i will contact you regarding this mange mungu akubariki
jamani
lol   |2012-01-31 21:37:46
SISTER UMEZIDI KUWA BROWN DUU!! HOW IS UR HUBBY? I MEAT HIM AND I WILL NOT TELL
U WAPI IT IS MY SILI.
Anonymous   |2012-02-01 06:23:47
english course is calling...
LiZZie   |2012-02-02 16:40:18
Indeed...
Anonymous   |2012-02-01 07:34:12
I meat....kwiiii kwiiiii
JUDITH   |2012-02-01 09:55:09
TOA MCHANGO HABARI ZA HUBY WAKE HAZIKUHUSU BROWN BROWN YA NINI????PESA MBELE
KWANZA NDIO TOA SALAM ZAKO MBUZI WE
mdau usa   |2012-01-31 21:55:59
Huyo kaka alokula pesa za watoto za juice na biskuti ukimuona tena mnyie mbovu
yake mamake usimuache ili aone aibu ajue alichokifanya sio kizuri.
Anonymous   |2012-01-31 23:46:24
as much as we talk about u YOU ARE DOING A GREAT THING for these children.
Yani I dont know why u feel the need to do this but i thank GOD that u have the
desire to reach out which is more than any of us in here are doing and to think
that we are ALL blessed with so much...saa nyingine natamani kulia bc of how
selfish us human can be. Please please keep u the good bc those children sure do
need it! MUNGU AKUBARIKI
Anonymous   |2012-02-01 00:08:18
niko nchi moja ni maskini sana ila huwezi kuamini wako very honest
wanavyosaidiana mpaka raha...ila nchi yetu Tz, watu wako very selfish, walafi
wanajali familia zao tu bila kujali wengine na kwa hili we have long way to
go....nasikia uchungu sana ila ndo hivyo tena sina sauti yaani inasikitisha sana
subira   |2012-02-01 03:15:49
Mange you are making a difference in these kids' lives. God will really bless
you for that. Ni wachache kati yetu wenye moyo kama wako. Waking up leaving your
luxurious life and kids at home and go to these kids. Mungu atakulipa hapa hapa
duniani. Don't give up on them. Hao wanaokula hela za watoto wasikuvunje moyo
DJ   |2012-02-01 03:26:28
Tuzidrop wapi hizo nguo bibie, nina nguo za watoto saizi hiyo nyingi na viatu
pia, nimeanza kuziandaa kwa kuzifua na kupasi. le me know..Hongera sana Mungu
akuzidishie baraka tele.....
Parrot   |2012-02-02 02:58:14
nguo na toys zipelekwe Kiki's pale mikocheni opposite tanesco.
Anonymous   |2012-02-01 03:31:28
Mange ulipewa ruhusa kutangaza status ya huyo mtoto?
Shaban Myonga  - Hongera mange   |2012-02-01 03:42:32
Yaan Sis naona mimi binafsi machozi yamenitoka kwa yule mtoto mwenye ugonjwa wa
ngozi na jinsi walivyochakachuliwa kwenye juice na biscuit, ndio uone wabongo
walivyo usemi wa kutowapa pesa mimi naona ni sawa kabisa.
Mange na mwenyezi
mungu atakufunulia kwako mambo yako yote yaende vizuri kwa moyo wako wa upendo
kwa hichi ulichokianzisha nakuombea sanasana nimekupenda saaana! Mama Bhokenzo
S MU  - no   |2012-02-01 03:45:01
Hi Mange,

Hongera, naomba Mungu azidi kutufungua tuwasaidie wanauhitaji kama
hawa watoto.

Ushauri wangu hizo kanda mbili kwa watoto huwa zinakatika haraka
kutokana na kucheza, nashauri zinunuliwe yebo yebo fulani hivi za kuingiza tu
mguu huwa zinadumu.

Kila la kheri.
Farida   |2012-02-01 04:07:36
Mange my sister.. Mungu akubariki kwa kweli..

Ila mimi naona badala ya
kandambili ambazo watoto wakicheza wanazipoteza haraka, kwa nini usinunue
crocs-zile za kawaida tu za bei ya chini ili wawe wanazivaa mguu unaingia
kabisa, hizo naona zitawasave kidogo maana kwa watoto naona kandambili ni rahisi
kuvua.

Halafu kwa hiyo misaada, mamii nunua kila kitu na uwape watoto wenyewe
sio kukabidhi watu, la sivyo hawataviona. ikiwezekana wapeni surprise siku
chache after hiyo event muone kama wanawapa watoto whatever
mmewapelekea.

Mange Mungu akupiganie tu, May He bless you mpaka ushangae.....
c's mum!   |2012-02-01 04:16:33
kilio kikubwa kama mdau hapo juu, MUNGU JUU MUUMBA, awaondolee watoto adhabu ya
ukimwi maana hawastahili mateso haya, MANGE MUNGU AKUZIDISHIE!
Anonymous   |2012-02-01 04:36:14
MANGE NINA SWALI, KWANI HIVI NI LAZIMA NICHANGIE KABLA YA SIKU HIYO NDIO NIPATE
NAFASI YA KWENDA HUKO AMA NAWEZA KUJA NA MICHANGO YANGU SIKU HIYO HIYO?? MAANA
NATOKEA NJE YA DAR SO INANIWIA VIGUMU KULETA MCHANGO WANGU(AMBAO SIO HELA) NA
KURUDI TENA HUKU THEN KUJA TENA HUKO DAR. NATAKA NIKIJA NAKUJA NAO KBS
JUMLAJUMLA.
Anonymous   |2012-02-01 06:49:55
kama upo serious wasiliana ane kwenye email yake ama simu yake aliyoitoa ya
mpesa,
Anonymous  - re:   |2012-02-01 04:55:22
Mimi ninachokiona hapa, hizi Ophanage center wanawadhalilisha hawa watoto ambao
wameamua kwa hiari yao kuwahudumia. Hainiingii akilini kama unavyoona watoto
hawana viatu, nguo chafu wanatofauti gani na wale ambao wanazunguka barabarani
kuomba. Hizi center zinapata misaada mingi sana kutoka sehemu mbalimbali
nafikiri huwa zinaishia mikononi mwa wamiliki. Kama hali inaonekana hivyo katika
mavazi, chakula je?

Au wanavalishwa hivyo kwa mtego kwamba kuna wageni
wanakuja kutembelea then waone kuwa kuna shida kubwa, hakuna fedha, kwa hiyo
watakuwa na huruma na kumwaga fedha ambazo hazitawasaidia hawa
watoto.

Nafikiri pia kama kuna wizara husika ifuatilie kuangalia hawa
wamiliki wanaopewa leseni za kuendesha hizi center, are they doing what their
supposed to do. au wamekaa pale kudaka hela za misaada kwa manufaa yao.

Huyo
mtoto mwenye vipele kama ameungua ametibiwa? hawezi kuambukiza wenzake ? hawa
wamiliki are they profes...
Anonymous   |2012-02-01 05:02:54
We've got twiga stars,mwamvita makamba wth her foundatn,mange kimambi wth her
project,flaviana matata, khadja m'mboka n the list goes on n on, tz women
changing lifes,gota love them

Could nver ask for more, keep up the good wrk
mange n all the women out there
Anonymous   |2012-02-01 05:49:51
Watanzania tunatakiwa kuelewa kuwa unapokuwa mgonjwa c wa HIV ht malaria
unahitaji care je unapokuwa muathirika tena mtoto utakuwa na mahitaji kiasi gn
upate special diet matunda usafi ucmamizi wa matumizi ya ARvs iwapo kituo hicho
kina mtoto mmoja tu wa aina hy nani atamcmamia anony wa kwanza yupo right kabisa
nimeumia sana roho na hy mtot pls wenye kujua vituo vya kulea yatima waathirika
pls watoe msaada na huyu afikishwe huko. Mchango wangu ni maombi
MANGE STAY
BLESSED
Mama D   |2012-02-01 06:26:16
Mange kuna kitoto kingine kiko mwanza ni yatima na anangoma na anaishi kwa
kuomba omBa, ushauri ni kwamba hizo pesa Za karo utakuwa unawanufaisha wahusika
kwani ela ya serikali ikija wataweka kibindoni Vipi ukienda mwanza ukampa mkono
wa furaha yatima yule na shida yake kubwa huwa nidawa ya ngozi ambayo alidai
inauzwa 40,000 km ckosei. Muulize rafiki yako Joyce ndo alimrusha kwenye mimi na
Tanzania. Niombi tu waweza Li yes au Li no. Sijachanga vile ninasomesha watoto
yatima 5 sekondari vyuo na primary thats y ila nitaenda kitembelea kitoto hicho.
Mungu awaondolee watoto adhabu ya UKIMWI amen. Mungu ivariki Tanzania na sisi
pia.
Anonymous   |2012-02-01 17:36:20
mama D huyo mtoto ni wa kiume?kama ni yeye yupo pale nje ya airport ya mwanza
anatia huruma sana,yule mtoto aliniliza lakini kila siku yule mtoto anaomba pesa
sasa sijuhi analelewa na nani?
MFUFU  - THINK BEFORE YOU ACT!!!   |2012-02-01 06:50:32
POSITIVE THINK!!!
Well Mange your idea ya kuwasaidia watoto especially
kituo kimoja ni nzuri sana.
WHERE YOU WENT WRONG!!!
But ulitakiwa after
choosing hicho kituo theeeeen ungefanya plan a) kuongea na wakubwa wa ustawi wa
jamii au wizara ya maendeleo na watoto (whatever) wakupe some rights za
kudumisha idea plan yako( meaning if something went wrong in the center and you
know you have a right' someone ass must be purnished)
You needed a person who
grew up in this chaos to tell a story!! produce TV document Behind the scene(
and Kids too must be part of the doc.)
REMEMBER!!!
The goal
is to create a sustainable development, so other centers could also learn from
it.
WHO TO BLAME FOR THIS!!
The system who hired cheap labor in
the center, the have no experiences what so ever, no body cares to recognize
them, if they are doing good job or not, money(caching) becomes no.1 moti...
Anonymous   |2012-02-02 04:26:46
unashindwa nini kufanya wewe hayo unayoona ni sahihi unasubiri watu wafante uje
kukosoa. hao uustawi wa jamii ni kazi na wajibu wao hawahitaji Mange akawaambie
watoke wenyewe maofisini wanakoshinda wanakula vitumbua wakafanye kazi.
Anonymous   |2012-02-01 07:01:31
Hivi Mange huyo kaka aliyekula pesa ni yule uliyemsifia sana, kuwa tutamuona
tutamuona. Kakuonyesha side yake ya pili?
Anonymous  - Let us do something for March (Womens' day)   |2012-02-01 07:02:20
Dear Mange, i'm the one who proposed you to be invited for wanawake live show.
My intention is, to let you sensitize the Tz communities on caring others by
using the Valentine event. Watu wengi hudhani Valentine ni ya wapenzi tu. Mungu
akubariki sana kwa hili, mimi naguswa sana na hii issue.

Je utaweza kuiangalia
pia siku ya wanawake duniani 8/3/2012. Naomba kuwe na event hata kama ni debate,
kuna wanawake wengi waliokata tamaa, kiuchumi, magonjwa, unyanyasaji, dhuluma
n.k. Kama tusipopeana moyo na kuhamasishana hatutajikwamua katika baadhi ya
niliyoyataja. Najua uko creative. Please do something.
madam bbm   |2012-02-01 07:33:00
ushauri tu....siku nyingine ukiwa unaenda kutembelea kituo chochote
hakikisha unabeba vitu kama juice/soda.unatoka navyo home kabisaa.idadi ulikuwa
tayari unaijua. manake vijana sasa wamedata na uchumi
kigenda   |2012-02-01 07:41:43
Hi Mange
Hiyo story ya watoto kutokununuliwa soda imenitourch, hii
ina confirm kwamba baadhi ya watanzania wenzetu hawana utu hat kidogo. Huyo
jamaa ana roho ya chui, hata kama anajifanya anafanya kazi hapo. Wakati mwingine
utajiuliza jee watu hawa wanafanya shughuli hizo kwa mapenzi au ni faida zao
wenyewe. Basi namuunga mkono aliyesema kwamba usipeleke cash nunua vitu uwaachi.
Na hata hiyo kuwaachia vitu inabidi mara kwa mara upite kuhakikisha bado vipo la
sivyo vitapigwa mnada. Lol watu wana njaa
Anonymous   |2012-02-01 14:49:06
Imekutourch???duh.ungesema tu imekugusa.
jef  - DHAMBI YA KUCHAKACHUA....     |2012-02-01 08:13:58
Unachofanya ni mpango wa Mungu aliotuagiza sisi wana wa Adam tuutekeleze, na kwa
kufanya hayo ndo tutakuwa tumempendeza.

Mambo mawili ambayo nimeya observe
kupitia moja ya kituo cha watoto yatima uliotembelea, ambayo nahakika yanaleta
madhara makubwa kwa watoto ni:

1. UTU, HURUMA NA UAMINIFU KWA BAADHI YA WALEZI
VITUONI;
Umejionea mwenyewe, tena baada ya kushushuliwa na watoto wadogo ati
wewe ni miyayusho ktk miadi yako. Kumbe pesa kaachiwa mlezi atimize lile
ulokusudia na akaingia mitni na pesa bila hata chembe ya huruma kwa hao
watoto.

Si huyo tu, vituo vingi havifikishi misaada kikamilifu kwa watoto wa
jinsi hiyo, badala yake watu wenye roho ngumu wana andika proposals nzuri kweli
kweli na wanapewa pesa nyingi tu ambazo zingeweza kuwasaidia watoto ktk mahitaji
mengi muhimu ikiwa ni pamoja hizo ndala utakazo wapelekea.

Dhambi ya
kuchakachua inalitafuna sana hili Taifa. Simpo, mnyime mtu Elimu na Exposure
utampeleka u...
Anonymous   |2012-02-01 08:44:45
dada myeyusho lol
Anonymous   |2012-02-01 09:20:25
Mange, naomba nikupe hongera kwa utayari wako na moyo wa kujituma kuwasaidia
watoto yatima. Lakini naomba nikufungue macho, watanzania wengi sasa hivi
tumekuwa walafi na wabinafsi. Kwa hiyo unapotoa msaada kwa hawa watoto kama
unaweza (kama ulivyofanya kwa ofa ya juice na biscuit safari ya jana) hakikisha
ulichopeleka kinagawiwa watoto. Watu hawana huruma, usishangae hata vitu
mtakavyoenda navyo hiyo tarehe 12 watoto wasipate hata kimoja. Mabox ya sabuni,
mifuko ya michele etc vyote vitavushiwa majumbani kwa hao walezi wa watoto.
Unajua unaweza ukasema watanzania wenye nacho wana roho za uchoyo kwa jinsi
wasivyokuwa tayari kupeleka misaada kwenye hivi vituo, la, ni mambo kama haya
ndyo yanawalazimisha watu kuwa wagumu kutoa. Nina hakika kama siyo uchakachuaji,
watoto wa hiki kituo wangekuwa na maisha mazuri kama yale ya watoto wa kituo cha
msimbazi. Shida wizi, hakuna uaminifu, upendo na kujaliana. Kazi tunayo kubwa
sana Mu...
Anonymous   |2012-02-01 09:32:24
mange katika harakati za kutangaza jina na kugombea ubunge miaka ijayo
Anonymous   |2012-02-01 10:25:50
Nina maoni kama michango itakuwa ya kutosha basi wangenunuliwa washing machine
ili wasiwe na nguo chafu,pamoja na viatu hata vya mtumbani,na sox atleast wawe
kwenye mazingira masafi kuzuia maambukizo yasiyo ya lazima,huyo dada wa hiv
anunuliwe centrodem crem atapona after 3 to 5 days
Anonymous   |2012-02-02 09:02:52
washing machine ni wazo zuri ila bongo maji shida mashine itadoda bure!
matem   |2012-02-02 06:21:54
DEAR MANGE MI NITATOA DAWA ZA MTOTO,ETI MPAKA SASA HIVI SIJAJUA MISAADA
INAPELEKWA WAPI : : MAKUBWA MIE,MSINICHAMBE JAMANI
matem   |2012-02-02 07:22:45
mange unafanya mambo matam kama baga ya morocco
Abi  - ABI   |2012-02-02 08:04:04
Mange mimi huwa si comment kwenye post zako mara kwa mara but hili limenigusa
sana, katika kitabu cha Mungu kinasema Dini iliyosafi ni kwajali YATIMA... you
are doing a right thing, Mungu akubariki..... BIG UP
Anonymous   |2012-02-02 09:48:52
Bless u Mange for the outreach. Ila kitu kimoja I would call it "HEADS
UP", hiyo issue ya huyo kaka kula hela ya soda za watoto inaonesha jinsi
gani hapo mahali uchakachuaji umekithiri. Naona ni vizuri kuwe na action plan
kwa ajili ya control ya michango yote inayotarajiwa kupelekwa hapo. Siyo tuu
financially but also material support. Watu kama hao wanaweza hata iba nguo na
malapa ya watoto. Nashindwa hata kusema nishauri nini kifanyike kwa case kama
hii but labda kuna mtu akisoma hii coment yangu atapata inspiration ya action
plan for this. Wadau pls lets think abt it!
wa mtoni   |2012-02-02 15:34:31
Mange umebana comment yangu lakini I hope ujumbe umeupata!!
Hs   |2012-02-03 10:25:10
Mange hongera sana dadangu, unapata dhawabu sana mashallah! I wish also i can do
any help!! Mashallah
kim kardash   |2012-02-03 17:22:24
je watu wa wizara ya jamii wanawake na watoto inafanya nini kumsaidia mange na
watu kama yeye,si ajabu hata pale airport dar akishuka wanampiga ushuru na vitu
vyake kama kawa wakati anajitolea kwa ajili ya jamii
Write comment
Name:
Email:
 
Website:
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
:confused:8):lol::x:P:oops::cry::evil::twisted::roll::wink::!:
:?::idea::arrow::blink::dead::coffee::karate::gossip::hahaha::newpost::love::lips:
:no::nono::rofl::shrug::stop::tape::thumbsup::wail::waves::yahoo::yes:
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

 
 
Follow Mange on Twitter
Find U turn Blog on facebook