Who's Online
We have 337 guests online
Total number of Visitors
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday6845
mod_vvisit_counterYesterday8768
mod_vvisit_counterThis week6847
mod_vvisit_counterLast week82441
mod_vvisit_counterThis month53919
mod_vvisit_counterLast month319970
mod_vvisit_counterTotal No. since we started4933486
Login



MSAADA WA KUANZISHA BIASHARA...
Written by Mange   
Tuesday, 17 August 2010 19:49

Mimi ni mama  wa 2 kids nahitaji kuwa mjasiliamali .

Nina mtaji wa Tsh 5,000,000.00 tu nataka kuanza Biashara  angalau na mie nijikwamue kimaisha

Nashindwa nianzie wapi hapa dar kupata kibanda gharama na Bei kubwa ambayo itanimalizia mtaji wote

Kina  dada / mama / baba wenzangu nipeni mawazo nianzie wapi mie  nimechoka kuwa tegemezi  nahitaji kutoka  natamani sana .

Dada mange usiweke mail yangu. Kama kuna mtu atahitaji kuwasiliana na mie nitampa

regards

Comments
Add New Search
Anonymous   |2010-08-18 03:30:27
Whooou safi sana mamii.....kwa mtaji wa milino 5 ni mwingi sana kama una nia
utafika..muhimu uwe na soko tu la bidhaa zako....lakin kuhusu frame maeneo ya
kinondoni/sinza frame zinaanza 150,000 kwa mwaka 1,800,000 katika 5m itabaki
3,200,000...labda wewe ndo utuambie umefikiria biashara gani unaona inaweza
ikatoka kwa hapo dar.....

Mie msaada ntakaokupa kama kuna bidhaa ambazo
utataka kuuza na zinapatikana kwa dubai...basi nitakusaidia kukununulia na
kukutumia (kama utaniamini)....
Anonymous   |2010-08-18 19:10:03
Mama uturn naomba hicho kikopo chako usituonyeshe kwenye picha kinatia kinyaa,
naogopa siku hizi kuangalia picha zako nikikiona tu nafunga blog na umbea
kwishney. Ni ombi tu dada unatukwanza wengine. Asante :)
Anonymous   |2010-08-18 05:03:15
mambo,
Hongera kwa kutaka kuwa na kipato chako thats a very good willl; Tatizo
ni kwamba value of money ya sasa inazidi kushuka, kuna miaka kama ungekuwa na
hiyo 5M ungefanyia kitu cha maana lakini sasa duh, hata pango tu ni la miezi
miwili - anyways tuachane na hayo
A few ideas;
1. explore swala la direct
sales - jiunge na oriflame, au forever living kama unaweza kuongea utauza
directly na ofisi inakuwa kwenye mkoba - they pay ukiwa serious na mtaji si
mkubwa.
2.Food staff - kama upo dar tembelea ma ofisi unachukua order ya
chakula unapika from home una supply b/fast & lunch.
3.Choma tofali - uuzie
wanaojenga - unakodi eneo vijana wanachoma then unauza
Naendelea kufikiria -
vingine kuna biashara nyingi ila kwa ww mtaji unakulimit...tupo pamoja
eshe   |2010-08-18 06:57:33
Dada kwanza honera kwakuwa ni wanawake wachache sana wenye mawazo kama yako. Ni
vizuri kutokuwa tegemezi kwakuwa la kesho hilijui.

Sasa cha kwanza cha muhimu
ni ujiulize unauzoefu na biashara gani japo kidogo. Kwasababu biashara zipo
nyingi tena sana ila swali ni je unauzoefu japo kidogo?
Kwakuwa kuna madhara
mengi kufungua biashara ambayo huna uzoefu nayo kabisa kuna uwezekano mkubwa wa
kuyumba na hata kupoteza mtaji wako. Hivyo hilo ni la kuliangalia.

Pia kuna
biashara ambazo ukiwa na mtaji huo unaweza kumudu mfano. Kufungua KI-CAFE ambapo
utakuwa unauza soda, maziwa, chai, keki maandazi na vitu kama hivyo na bado hapo
mbele ya banda lako ukamuweka mtu wa chips uwe anakulipa kwa comission.

Pia
kasaluni kadogo dogo au hata duka la kuuza maji na juisi za jumla. Huo ndo
ushauri wangu.
Anonymous   |2010-08-18 07:31:01
dada fungua duka la building materials ie hardware tofauti tofauti na
electronics hautajuta pango weka nje ya mji karibu na watu wanaojenga kimara
barabara kubwa kuzuri tafuta centre nzuri iliyokaribu na barabara za ndani
ambako watu wanajenga halafu hautalipa kodi kubwa sio zaidi ya 100,000 kwa mwezi
nakuambia linalipa saaana, niamini mimi ndio biashara yangu na mambo yangu si
mbaya ninayo mawili sasa, usihangaike na biashara za saloon sijui botique kama
wewe sio fashonista au hauna hobby, utajuta nilishajaribu nikashindwa. hope
itakusaidia.
Anonymous   |2010-08-19 06:23:04
saloon boutique pia iko very congested
asha  - Ms     |2010-08-18 08:45:31
i have never commented before on this blog but i am impressed that women
are taking risks and venturing into biashara.

I would advise you
to do your research before doing anything,get into something that you
have an interest in as passion is important,then analyse the market and
check out what your competitors are doing,whats working for them and
whats not working for them,

i would advise in offering something
unique,and in high demand so that you can ensure your
business services are always in demand,focus on offering value for
money and quality.

Rent is exorbitantly expensive in Tanzania hence
starting a business using your networks (friends,friends
of friends,family,etc),use your phone to advetise,send out emails to
potential customers,set up an online store (this will obviously also
depend on your target market and if they...
Josepher Muru  - JINSI YA KUANZA BIASHARA   |2011-09-16 10:26:22
Wadau wa blog hii,habari za mahangaiko,mimi ni mjasiriamali na pia natoa mafunzo
kwaajili ya watu wanaopenda kufanya biashara kama mimi ,ninampongeza mama kwa
mwamko na moyo alionao,ninachoweza kumshauri mama atafute muda wa kuja kwenye
mafunzo kama atapenda kujifunza mbinu za biashara na biashara gani mtu anaweza
kufanya kutegemea na kipato alicho nacho,kuhusu mafunzo wasiliana nami kwa no
0786020703/0656020703
LuluRenee  - Msaada     |2010-08-18 09:14:14
Nakushauri utafute eneo zuri uanzishe biashara ya chakula, unaweza kutafuta
maofisi ukawa unawapelekea lunch kwa order au ukawa na eneo unapika chakula
kizuri watu wanakuja kununua. Kila mtu lazima ale kwa hiyo biashara ya chakula
inatoka. Ukiona hupendi kuwa mama lishe basi kama upo Dar ingia kariakoo, nunua
handbag, viatu, na accessories na hata vitenge halafu unakuja kuuza maofisini.
Sisi tuliopo naofisini mara nyingi hatuna muda wa kupita kariakoo kwa hiyo
hatufanyi shoping. Say ukinunua handbag ya 15,000 ukauza 20,000 hujapata hasara.
Kama unaona hata hiyo huitaki basi peleka DESI zikawe mbegu, zikiiva utavuna
matunda.
Anonymous   |2010-08-18 10:18:56
Leo nilipo kuwa nakula nilikaa na mtu ambaye amenipa idea ya biashara... i dont
know how expensive it is but since ww unatafuta idea za biashara it's worth
exploring na hii utaifanyia home my dear - ya kufuga mbwa get good dogs and
start breeding them trust me you will sell.
best of luck
mwenye nia   |2010-08-18 10:19:00
wapenzi asanteni sana kwa mawazo yenu ni mazuri sana ,..kuna mmoja amenishauri
nifanye biashara ambayo nimewahi kufanya ..sijawahi kufanya biashara yoyote ndo
maaana nadhani mtandao huu unatembelea na watu wengi wafanya biashara .ndio
maana nategemea mawazo yako kwa wingi
mwenye nia  - re:   |2010-08-18 10:21:23
Anonymous wrote:
Whooou safi sana mamii.....kwa mtaji wa milino 5 ni mwingi sana kama una
nia utafika..muhimu uwe na soko tu la bidhaa zako....lakin kuhusu
frame maeneo ya kinondoni/sinza frame zinaanza 150,000 kwa mwaka
1,800,000 katika 5m itabaki 3,200,000...labda wewe ndo utuambie
umefikiria biashara gani unaona inaweza ikatoka kwa
hapo dar.....

Mie msaada ntakaokupa kama kuna bidhaa ambazo utataka
kuuza na zinapatikana kwa dubai...basi nitakusaidia kukununulia na
kukutumia (kama utaniamini)....


nakushukuru sana dada kwa mawazo mazuri nayafanyia kazi ..asante god
bless u nitahitaji contact zako nitaomba dada Mange akupatie
Anonymous   |2010-08-18 10:23:03
@ anonymous, unasema afungue duka la vifaa vya ujenzi, naomba utuchanganulie
huo mtaji wa 5M?? pls
mwenye nia   |2010-08-18 10:24:10
asha nashukuru kwa mawazo yako mpendwa nitaanza hiyo research ASAP na nitarudi
kwa mange kutoa feedback kwa wote wanaonipa ushauri
Anonymous  - re: Msaada   |2010-08-18 10:37:45
LuluRenee wrote:
Nakushauri utafute eneo zuri uanzishe biashara ya chakula, unaweza kutafuta
maofisi ukawa unawapelekea lunch kwa order au ukawa na eneo unapika
chakula kizuri watu wanakuja kununua. Kila mtu lazima ale kwa hiyo biashara
ya chakula inatoka. Ukiona hupendi kuwa mama lishe basi kama upo Dar
ingia kariakoo, nunua handbag, viatu, na accessories na hata vitenge halafu
unakuja kuuza maofisini. Sisi tuliopo naofisini mara nyingi hatuna
muda wa kupita kariakoo kwa hiyo hatufanyi shoping. Say ukinunua handbag ya
15,000 ukauza 20,000 hujapata hasara. Kama unaona hata hiyo huitaki
basi peleka DESI zikawe mbegu, zikiiva utavuna matunda.



mh! deci? lol sishauri kwanza ilifia wapi??
Anonymous   |2010-08-18 11:49:27
Desi, ???????????????!!
Anonymous   |2010-08-18 12:42:00
Huyo Asha hapo juu hana lolote, mama katuma message kwa kiswahili yeye anatuma
kwa kiingereza, who the hell do you think you are? get a life. Ni hivi,
nilianzia mbali kuanza biashara, nilianza na kupanda mapassion, maaloe vera na
kusupply kuku kwenye mahotel makubwa kipindi hicho na mtaji wangu ulikuwa mdogo
tu . una mtaji mkubwa, anzia huku kila unachopata unasave, mpaka nilipo,
ninauza vinyago na nimekuja kusoma huku uingereza kwa biashara yangu hii
mpaka sasa siiachi kamwe.
Anonymous   |2010-08-18 13:02:50
SHOST CHUKUA IDEA HIZO UINGIE BARABARANI TULIENDEKEZE LIBENEKE LA
UMACHINGA.
WADAU NAUZA SAMAKI WA MWANZA WALE WA KUKAUSHWA! YEYOYE ANAETAKA
ASEME NTAMPA EMAIL/NO YANGU, NAKULETEA MPAKA MLANGONI KWAKO, PIA MDAU HATA HII
NI NZURI UNANUNUA SAMAKI KUTOKA MWZ UNAWAUZIA WATU WA MAOFISINI TU. UNAKUWA NA
VIJANA WAKO WANAKUSAMBAZIA WEWE UNATAFUTA ODA. MTAJI KIDOGO FAIDA KUBWA THOUGH
IT HAS HIGH RISKS!
shaeli  - msaada wa kuanza biashara   |2010-08-18 13:41:33
unaweza kufuga broiler na wanafaida nyingi,ila itabidi uwe msafi,wakiumwa wahi
dawa,nunua chicks kwenye company,najua utaoga kwasababu utakuwa ushasikia kuwa
wanakufa sana,kiukweli watakufa kama unazembea,mi ndo biashara yangu since 2004
na nilianza na chick 500 leo nina 3000 napishanisha coz nina mabanda,kiukweli
hakuna biashara isiyokuwa na hasara,muhimu ni kusema hii ndiyo kazi yangu,kuku
ni kama watoto wadogo wanahitaji uangalizi
Anonymous  - re: msaada wa kuanza biashara   |2010-08-19 04:35:09
shaeli wrote:
unaweza kufuga broiler na wanafaida nyingi,ila itabidi uwe msafi,wakiumwa
wahi dawa,nunua chicks kwenye company,najua utaoga kwasababu
utakuwa ushasikia kuwa wanakufa sana,kiukweli watakufa kama
unazembea,mi ndo biashara yangu since 2004 na nilianza na chick 500 leo
nina 3000 napishanisha coz nina mabanda,kiukweli hakuna
biashara isiyokuwa na hasara,muhimu ni kusema hii ndiyo kazi
yangu,kuku ni kama watoto wadogo wanahitaji uangalizi

nakubaliana nawe Shaeli kuhusu broiler mimi ni m/ume na mke wangu anafuga
broiler tulianza na mtaji mdogo sana kama milioni 1.5 mwaka
2005 Kimara ila kwa sasa biashara yake imekua sana mpaka amenunua
pikipiki 5 za biashara (nazo zinalipa) na anaendelea na kuku ila inataka
moyo sana kuku akiumwa na wewe unaumwa kama ulivyosema Shaeli chakula
tunatengeneza wenyewe na tumenunua mashine kabisa za kusagia na...
Anonymous  - re:   |2010-08-18 17:25:29
Anonymous wrote:
SHOST CHUKUA IDEA HIZO UINGIE BARABARANI TULIENDEKEZE LIBENEKE LA
UMACHINGA.
WADAU NAUZA SAMAKI WA MWANZA WALE WA KUKAUSHWA!
YEYOYE ANAETAKA ASEME NTAMPA EMAIL/NO YANGU, NAKULETEA MPAKA MLANGONI
KWAKO, PIA MDAU HATA HII NI NZURI UNANUNUA SAMAKI KUTOKA MWZ UNAWAUZIA WATU
WA MAOFISINI TU. UNAKUWA NA VIJANA WAKO WANAKUSAMBAZIA WEWE UNATAFUTA
ODA. MTAJI KIDOGO FAIDA KUBWA THOUGH IT HAS HIGH RISKS!


Mmegeuza huu ni uwanja wa ubao wa matangazo ya biashara yenu? toeni
ushauri acha hizo mbwembwe za matangazo hapa.
Anonymous   |2010-08-19 11:02:47
unalo bibi!!!! mwenzio anaongea mambo ya maana unamshushua. poleeeeeeee
Anonymous   |2010-08-18 17:33:48
Habari Mange, huyu mama angeanza kwanza na biashara ya kawaida kama kuuza duka
inalipa akina bakhresa walianzia huko. huyo dada hapo juu anayeuza vinyago nae
alianzia chini hukohuko, kuuza vinyago nje inalipa mbaya sana. anza na duka ili
ubakishe japo hela ambayo unaweza ukainvest kwenye shares na makampuni tofauti.
usirisk kuweka hela yako yote kwenye biashara, pima kwanza,
Anonymous   |2010-08-18 17:40:52
ANZISHA JUICE & SNACK BAR, POPOTE INAUZA, JUICE FRESH, VIPOCHOPOCHO... VITAFUNIO
VYA CHAI , KACHORI,KEKI, BAGIA N.K. ALL THE BEST
Anonymous   |2010-08-18 19:34:14
Mdau aliyesema desi nimecheka hadi tumbo linauma na huku uswahilini usiku huu
wanadhani chizi nacheka mwenyewe! ila umejitahidi kutoa ushauri, mdau natamani
nikushauri kwani umeleta topic nzuri badala ya za umbea ila me nimezoea
kuajiriwa tu na still natafuta biashara hizo idea nami nacopy nikiwn i wil be
back to uturn na sucess stor, ...........niko nje ya mada!!!
Anonymous   |2010-08-18 23:50:57
mi napenda kuwashukuru wanawake wenzangu wote mliochangia jmn mimi nafanya
biashara ya kuku japo haija changanya sn ila si sawa na kukaa bure naamini
ntafika mbali,swali kwa anonymous mmoja hapo juu uliyesema ulianza na
mapassion,kuku na sasa upo uk unauza vinyago,naomba ushauri niliuza vinyago
mwanzo kw muda2 nkawa napeleka slipway lkn nkaon haitoki kipindi cha watalii
nkawa naenda znz pia haikuwa nzuri sana ndo nkahamia kwny kuku,ila umenitia
nguvu uliponambia upo nje now na still unafanya hiyo,naomba nisaidie jinsi
yakupata soko inawezekana nilikuwa sijui soko lake liko wapi.mi niliipenda mana
havifi wala haviozi,nakutakia mafanikio uliyeomba ushauri usiogope jiamini.
Josepher Muru   |2011-09-16 10:12:17
wadau habari za mahangaiko,napenda kumpongeza Mama ambaye anataka kufanya
biashara,mimi ni mjasiriamali na pia natoa mafunzo kwa watu wote ambao wanataka
kufanya biashara ,kama mama unapenda kufanya biashara inabidi siku utafute muda
wa kuja kwenye mafunzo na mafunzo hayo yanafanyika bure ,kwa mawasiliano number
yangu 0786020703/0656020703.
Rosie  - Ms   |2010-08-19 06:05:33
Dada unaefanya biashara ya samaki wakavu wa mwanza naomba uweke contacts
zako,nawahitaji.
Anonymous   |2010-08-19 10:57:42
LOL! BORA UMENIPA MOYO MAANA NIMESHUSHULIWA PALE JUU MPAKA VIDOLE VINASHINDWA
KUTYP!
irene msangi   |2010-12-27 12:58:35
hallow dada rose. unahitaji samaki wangapi? my phone number is 0715111484,
0789111484, 0757111484. naitwa irene msangi pia najulikana kama mama gati naishi
mwanza.
irene msangi  - re: Ms   |2010-12-27 13:01:20
Rosie wrote:
Dada unaefanya biashara ya samaki wakavu wa mwanza naomba uweke contacts
zako,nawahitaji.


naitwa irene msangi pia najulikana kama mama gati. naishi mwanza, phone
numbere is 0715111484. unahitaji samaki wangapi?
DadaMkubwa   |2010-08-19 06:45:19
Jamani nimekubali mambo iko huku,
zamani watu walikuwaga wanasema eti wanawake
tuna roho mbaya hatusaidiani BUT sasa naona tumeamka,
Dada unayeuza samaki wa
Mwanza weka contact zako tuanze kukuagiza samaki,ofc zetu ziko upanga Dar

Napendaga sato wabichi
irene msangi   |2010-12-27 13:03:52
HALLOW DADA MKUBWA. NAITWA IRENE MSANGI, Naishi mwanza. you can kutafuta me by
phone number 0715111484.
Anonymous   |2010-08-19 07:09:33
mange mama kimya,,,,,,,,vipi tena?????? au ushaanza uchungu nini?? Maana
naimeona jiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!@!!! I PRAY 4 YOU,,,,,,,Ujifungue
salama mummy!!!!

Mi nakuonea huruma saaana......... but wanawake tuliumbwa
hivi kuzaa kwa uchungu!!!!!

MUNGU akutangulie.
Anonymous   |2010-08-19 11:34:10
Mange kashashusha injini nn mbona kimya sana humu?
Anonymous   |2010-08-19 18:05:44
biashara ingine nzuri ni ya chakula cha kuku,kinakuaga adim mmno mtaji wako
mzuri,mi nna mdada yeye alienda kusoma nje jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku
saizi ameweza kununua na machine ya kusagia hiko chakula na hawezi kuwaridhisha
wateja wake demand ni kubwa mno.kama uko interested ntakupa contact zake ni
mlokole hawezi kukutolea nje!!!
Anonymous  - re:   |2010-08-20 04:15:17
Anonymous wrote:
biashara ingine nzuri ni ya chakula cha kuku,kinakuaga adim mmno mtaji wako
mzuri,mi nna mdada yeye alienda kusoma nje jinsi ya
kutengeneza chakula cha kuku saizi ameweza kununua na machine ya
kusagia hiko chakula na hawezi kuwaridhisha wateja wake demand ni kubwa
mno.kama uko interested ntakupa contact zake ni mlokole
hawezi kukutolea nje!!!


ASANTE SANA MPENDWA MANGE NAOMBA ADVICE HAWA WATU WATAPATAJE CONTACT
ZANGU? NITAZITOAJE KWAO PLS
Anonymous  - re:   |2010-08-20 09:27:47
NA[quote=Anonymous]biashara ingine nzuri ni ya chakula cha kuku,kinakuaga adim
mmno mtaji wako mzuri,mi nna mdada yeye alienda kusoma nje jinsi ya kutengeneza
chakula cha kuku saizi ameweza kununua na machine ya kusagia hiko chakula na
hawezi kuwaridhisha wateja wake demand ni kubwa mno.kama uko interested ntakupa
contact zake ni mlokole hawezi kukutolea nje!!![/quote

]NAOMBA UNIPE MIE HIZO
CONTACTS ZAKE NATAMANI SANA KUFANYA BIASHARA HIYO LAKINI NDO SIJUI HIZO MASHINE
UNAPATA WAPI NA WALA SINA HAKIKA NTAANZAJE HIYO BIASHARA. TAFADHALI MDAU NAOMBA
HIZO CONTACTS ZA DADA MLOKOLE!!
Anonymous   |2010-08-21 09:35:20
unaeza uliza pia kwenye maduka wanayauza mashine hizi za kusaga au kukoboa uliza
mashine ya kutngenezea chakula cha kuku lazima watakuwa na ideas au nenda kwenye
hizi vyuo vya kilimo kama SUA waulizie kuhusu mashine za kutengenezea chakula
cha kuku pia, nina vyojua simfahamu huyo mama mlokole najaibu kusaidia uliza
mabwana shamba pia wizara ya mifugo na kilimo msaada watakupa
xhera  - IT   |2010-08-21 11:03:35
Jamani naomba contacts za huyo dada anayeweza kunisaidia elimu juu ya chakula
cha kuku.....mimi nina kama 7m hivi
Mamaa G     |2010-08-21 11:06:08
Habari dada,
Naomba unipe na mie hizo contact zake natamaniI sana kufanya
biashara hiyo lakini sijui hizo mashine ntapatia wapi alafu mie nasafirisha
dagaa wa chakula cha kuku labda naweza kumfanyia biashara yeye pia. Tafadhali
mdau naomba hizo contact za huyo dada mlokole.!
Kitobelo  - re:   |2010-08-22 14:02:13
[quote=eshe]Dada kwanza honera kwakuwa ni wanawake wachache sana wenye mawazo
kama yako. Ni vizuri kutokuwa tegemezi kwakuwa la kesho hilijui.

Sasa cha
kwanza cha muhimu ni ujiulize unauzoefu na biashara gani japo kidogo. Kwasababu
biashara zipo nyingi tena sana ila swali ni je unauzoefu japo kidogo?
Kwakuwa
kuna madhara mengi kufungua biashara ambayo huna uzoefu nayo kabisa kuna
uwezekano mkubwa wa kuyumba na hata kupoteza mtaji wako. Hivyo hilo ni la
kuliangalia.

Pia kuna biashara ambazo ukiwa na mtaji huo unaweza kumudu mfano.
Kufungua KI-CAFE ambapo utakuwa unauza soda, maziwa, chai, keki maandazi na vitu
kama hivyo na bado hapo mbele ya banda lako ukamuweka mtu wa chips uwe anakulipa
kwa comission.

BIASHARA YA CHAKULA HAIMTUPI MTU, kwani watu wanakula,
wanakunywa.kila siku inalipa sana, as long utakuwa msafi na mazingira yako
masafi na utauza vitu vizuri kutokana na mahitaji ya eneo husika, halafu mtaji
ni mdogo tu...
Asha m   |2010-12-08 11:17:58
Nimependezewa na hiyo biashara ya chakula cha kuku naomba unisaidie hiyo anwani
ya huyo dada jamani. wanwake tukomboke na sisi.
emanuelmadafa  - jJounarlst   |2010-12-29 08:30:37
mimi napenda sana mamabo ya ujasiliamali but sina elimu ya biashara nifanyeje
emanuelmadafa   |2010-12-29 08:32:07
NAOMBA KUPATIWA ELIMU YA UJASILIAMALI NAPENDA KUFANYA KAZI YA KUJIAJILI MWENYEWE
NISAIDIENI
KHIM MOOT/....//mjasiliamali-K  - Advice     |2011-04-14 08:40:11
: .la kesho halijualo nanii?
;) emanuelmadafa,kazi zipo kwani waitaji
na kutekeleza mara tu umepata wazo..........haijalishi kiwango cha hela
hunazo,ila kidogo au kichache unacho kimetosha kukupeleka hatua
mbele,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,usaidizi utapokea ila tu huwe mpole wa
kungoja............
Rehema  - Ntafikaje China na dubai ktk maduka ya jumla ya ng   |2011-05-20 11:36:36
Habari zenu.
Mimi nataka kwenda dubai na china ktk maduka ya fenicha na mapambo
ya sherehe,nguo na viatu,tatizo sijui mjiau sehemu gani ya mji wa china ndio
ntapata vitu quality na bei nafuu.
Pia sijui nikishafika huo mji wa China au
Dubai ntafikaje madukani na ntasafirishaje bidhaa zangu kuja Tz.
Naogopa
matapeli wa huko nikiwa kama mgeni.
naombeni msaada wenu.
nazeema kassam   |2011-11-14 22:44:24
hi mambo vp nakushauri utafute mtu wa kukufahamisha sehemu za kwenda
stella  - Mambo mseto   |2011-12-08 07:26:12
Nakupenda sana Mange you are hot women big up, napenda pia
biashara lakini sijui chochote juu ya biashara.
stella  - Mabo mseto   |2011-12-08 07:33:30
Nakupenda sana Mange or Mama kenzo you rae hot women big up. Napenda pia
biashara lakini sijui chochote juu ya biashara na nataraji kuanza kufanya
biashara ila naogopa kupoteza mtaji wangu.
Write comment
Name:
Email:
 
Website:
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
:confused:8):lol::x:P:oops::cry::evil::twisted::roll::wink::!:
:?::idea::arrow::blink::dead::coffee::karate::gossip::hahaha::newpost::love::lips:
:no::nono::rofl::shrug::stop::tape::thumbsup::wail::waves::yahoo::yes:
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

 
 
Find U turn Blog on facebook