Who's Online
We have 371 guests and 1 member online
  • Fleetaves
Total number of Visitors
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday6635
mod_vvisit_counterYesterday8768
mod_vvisit_counterThis week6637
mod_vvisit_counterLast week82441
mod_vvisit_counterThis month53709
mod_vvisit_counterLast month319970
mod_vvisit_counterTotal No. since we started4933276
Login



NATAFUTA MUME.....
Written by Mange   
Monday, 16 August 2010 20:11

Habari zenu wadau. Nina miaka 34, nimesoma nina kazi nzuri, na pia naamini ninavutia kiasi kama mwanamke.

Nimetoka kwenye familia yenye maadili,nimelelewa vizuri sina maskandal yoyote kama wasichana wengine wa mjini nina tabia nzuri nimekuwa na maboyfriend wanne tu maisha yangu yote, sielewi ni kwanini mpaka leo hii hajatokea mwanaume wa kunioa.

Sielewi tatizo ni nini, ushauri naotafuta ni hivi,nifanyeje niweze kupata mume? Akiwa mtanzania mwezangu au mzungu ni sawa tu.

Msinielewe vibaya sio kama nimekuwa desperate ila najisikia vibaya rafiki zangu karibia wote wameolewa na wana watoto nimebaki mimi kila mtu ananinyooshea kidole.

Kuna waanawake wengi mji huu wanatabia mbaya sana ila kila siku unasikia mmoja wao kaolewa,mimi sijui hata madisco ni mtu wa kwenda kazini na kurudi nyumbani yani nimelelewa kwa maadili mema.

Nisaidieni mwanamke mwenzenu

Kuwasiliana na uturn tuma email kwenda This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it

Comments
Add New Search
Anonymous   |2010-08-16 15:34:17
Inaelekea ulikuwa mtu wa kuchagua sana...........sasa imekula kwako umri umeenda
huo dada. Pole we endelea kuvumilia labda utakuja kupata mume mzunguuuuuuu.
Ibrah   |2011-03-24 08:06:12
We dada hebu njoo hata mie napenda na kama unataka mtoto hakuna tatizo nicheck
ktk 0712 901298
Anonymous   |2010-08-16 16:27:37
Wee dada wanaume wanne uliokuwa nao si mchezo ni wengi wala usijiliwaze kusema
"nimekuwa na wanaume wanne tu maishani mwangu" Sidhani kama ni sawa hata
kuwa na mwanaume mmoja ambaye huna uhalali naye wala usijisifie kwa hilo kama
vile hujatembea hovyo.

Ujue kuwa katika hao wanaume wanne uliokuwa nao
umejiharibia bahati yako wala usingalie hao unaosema wana tabia mbaya lakini
wanaolewa.Hata wewe ulikuwa na tabia mbaya kujiingiza katika mapenzi na wanaume
wanne tofauti.hao wanaume wamekuharibia kwa kiasi kikubwa sana kwani wanaume
wanasimuliana kila kitu na habari zako zilitapakaa kote kama una kijitabia
fulani hivi watajua wote.

hayo maadili mema uliolelewa nayo ni yapi hasa kama
uliweza kuhangaika na mamen wote hao??Subiria Mungu mwenyewe atakapokuhurumia.
Anonymous   |2010-08-16 17:44:30
We nawe hebu tuondokee hapa pambaf... Wewe unamsema mwenzio wanne unamkosoa
wakati wewe umeshakuwa na miamoja.. kwanza nenda ukajicheki sio kukaa kukosoa
watu hapa.. mtu anaomba ushauri mnaleta masihara..
Anonymous   |2010-08-16 18:26:46
Ighsh.. wewe nawe.. wanaume wanne unaona wengi? ndo nyie hypocretes... We
mwenyewe usikute ulikuwa nao 40...
Anonymous   |2010-08-17 10:05:02
wa 4 kwa umri wa huyu dada ni wachache saaana mie nipo 25 nshakuwa na 8 mpk sasa
na sio malaya..
Anonymous   |2010-08-16 16:28:47
wanaume wa siku hizi hawaangalii cha mkorinto wala mjukuu wa mtume, wanataka
fun. my opinion, u sound boring....mie mume wangu nilkutana naye bar, nilikuwa
nimepata kinywaji cha kutosha hata gari nikashindwa kuendesha ikabidi ani-drop
home.........been married for 10 years now.....
Anonymous   |2010-08-17 06:07:48
u are rite mdau!!!!! Mume unakutana nae popote!!! I am an outgoing
person,,,since enzi za shule!! I also met ma hsband in a Nite Club,,,,,yeye pia
outgoing ka mimi,,, naw we are hapily married for 6 yearz with twins.

sasa
wewe dada uloomba ushauri,,,,I guess uendelee kumuomba mungu wako, ishi maisha
yako ya kawaida, ila usijiisolate sana na jamii,, cmaanishi uende kwe makilabu
ya starehe Nah!!! Ila jichanganye,,,, hata na wafanyakazi wenzio mara ingine
mkimaliza kazi cio lazma ukimbilie kujifungia nyumbani,, hao wachumba utawaonea
wapi au watakuonaje, hata Mungu anasema jisaidie nami nitakusaidia,,,,,,
onyesha juhudi na utafanikiwa.

Huwezi jua Mungu kakuandikia nini so usiwe na
inferiority complex!!! Jiamini tu. Nina rafiki yangu almost ua age, she is
32,,,single, kazi nzuri, kapiga shule zake vema, na anaishi maisha yake to the
foolest, hajutiagi hilo la kutoolewa,,anaamini time ikifika mungu atampa ubavu
wake. So...
Anonymous   |2010-08-17 08:21:59
nakukubalia anoy very boring life she have mimi bwana wangu ananifataga club
kama hanioni na i am dirty beach and he love it kama unapenda kusoma vitabu read
why men marry bitches na kingine be a lady and a bitch unaboa unaishi kama upo
dunia ya 1920 .siyo kila saa suti ukitoka kazini tinga umini kata mbuga show
what yo mama gave you
Anonymous   |2010-08-17 10:06:20
kweli she dounds boring kwenda club haimaanishi maadili sio mema u need social
life! nani anataka mke mboaji>hata kwenda outing hataki yani kazi na
nyumbani?thts the reason y hupati mtu. kuwa active socially huna mtoto tuseme
labda anakuzuia (yani majukumu) mingle dadangu lasivyo utalalamika bure
Anonymous   |2010-08-16 16:31:33
Pole sana dada yangu!!

Kama ningejua uko wapi au kama unaweza kuweka contacts
zako hapa nitakuwa tayari kuanza mawasiliano nawe.Mimi nina 36 na nahitaji kuoa
baada ya kukata shule zangu.Kama uko makini na hili jambo basi weka contacts
zako nikubip.Umenigusa sana na nimeridhia sana maelezo ya maadili uliyolelewa
nayo.Let us take our charge and see what is in btn us.Look forward to hearing
soon from you!!
Anonymous  - re:     |2010-08-16 17:58:10
Anonymous wrote:
Pole sana dada yangu!!

Kama ningejua uko wapi au kama unaweza kuweka
contacts zako hapa nitakuwa tayari kuanza mawasiliano nawe.Mimi nina 36
na nahitaji kuoa baada ya kukata shule zangu.Kama uko makini na hili
jambo basi weka contacts zako nikubip.Umenigusa sana na nimeridhia sana
maelezo ya maadili uliyolelewa nayo.Let us take our charge and see
what is in btn us.Look forward to hearing soon from you!!

sio ubeep unatakiwa kupiga unaanza ubahili mapema hata hujampata jamani
lol
Anonymous     |2010-08-17 06:36:38
hahahahhahahahahhhaha
|E  - lol!     |2010-08-17 06:37:47
hahahhahahahahahahhahhahh!!!!
Anonymous     |2010-08-16 18:00:59
kwa wote waliolewa na wanaotaraji
Jikoni kuwa chief

Kitandani changudoa
Huyo naisi ndo mwanamke
alolelewa kwa nizamu zote na atapata mume mapema na ndoa itadumu tu km mdau
alokutana na mumewe Bar nimekufagilia sn sn sn
Anonymous   |2010-08-17 06:11:46
ww naweumenichekesha,, umbip tena badala ya kupiga??? :0

Usije kua
walewale,, unataka kumega tunda kisela alafu ule kona kisingizio mbona wenzio
wanne walimega na kusepa!!!!

Kama muoji ni heri,, ila wanaume wengi wa
kibongo fixxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx!! Wadada wengi wameshamegwa kwa style ya njoo
nikuoe,,alafu wakipata tundi kazi kwishny!!!

Judith upooo???? Nimekumiss
bigga   |2010-08-17 09:57:41
sasa si uweke contacts zako mdau??
Anonymous   |2010-08-16 16:38:22
Nakubaliana na mdau juu hapo lux lyk unataka mlokole, mama kwenda disco au
kujirusha kwa ujumla sio kwamba huna maadili km unavowaoona wale wanaoenda
kwanza huko ndo wanapata wakuwaoa si wanaume wote wanapatikana kanisani. and u
sim desparate ila hutaki kukubali.
Jiachie ,jichanganye sikwambii
uwe malaya la hashaa mana we ni home na kzini tu basi change ur life stlyle and
pole sn mungu atakupa tu may b tym yako haijafika
Anonymous   |2010-08-16 16:43:05
Kwa maisha hayo unayoishi eti home kazini hutoki wala nini usidanagenyike kwenda
disco au popote kuchil na frienda sio uhuni na wanaofanya ivo sio kwamba
hawajalelewa kwenye maadili tena na kuolewa wanaolewa we usie na mabo hayo bado
upo
Tena omba Mungu hata uyo mume ukimpata awe km wewe nyumbani
ukitoka ni kazini lahasha mama ndoa utaiona mbaya anyway utampata kanisani au
msikitini
Anonymous   |2010-08-16 16:45:15
Watu wengi wanaojiita wa maadili km wewe inatake tym sn kuolewa mana kila
anaekuja unamuona km hajatulia unataka mpole km wewe any way usikate tamaa kwa
bwana Yesu wapo utapata
monie  - reply     |2010-08-16 16:45:45
Sorry but to me you seem to be too inferior...Hutakiwi kukosa raha eti kwa kuwa
hujaolewa, live your life manake kama Mungu amekupangia kuolewa utaolewa na kama
hajakupangia hata uombe ushauri wapi haitatokea!

Umesoma, una kazi...shida
nini? Huna raha kisa hujaolewa, that's bad...You need to to Single, Attractive
and Beautiful (SAS) akitokea wa kukuoa basi na atokee na sio ujione uko
incomplete kisa hujaolewa!
Anonymous   |2010-08-16 17:15:32
stop thinking you are perfect , stop being afraid of making mistakes. Make your
story. Men dont like a perfect gal. acha dharau you will get married.
Anonymous   |2010-08-16 20:13:21
KAULIZE kwenye FORUM ya JAMII FORUM,huko kuna midume imesoma na hawana hata time
ya kutongoza wao siasa tu na maswala ya maendeleo,dada yangu alimpata mmoja na
hivi sasa anapeta london
Anonymous   |2010-08-17 12:14:09
sasa kama hawana time ya kutongoza dada yako alimpataje? au yeye ndo
aliyemtongoza? wale wa jamiiforum sidhani hata kama wana time ya kutiana, kwa
hiyo akimpata baada ya muda tutamuona tena hapa uturn anataka ushauri mume wake
hampi uroda
Anonymous   |2010-08-17 12:56:07
WANAUME WA JAMII FORUM HAWANA HATA TIME YA KUBADILISHA CHUPI WALA YA
KUCHAMBA.....
Anonymous   |2010-08-18 19:15:03
Jamii Forum ni VIBAMIA tu vimejazana, na mambo ya alamba sio yao
inanhuuu????????
Anonymous  - re:   |2010-08-16 21:42:23
Anonymous wrote:
wanaume wa siku hizi hawaangalii cha mkorinto wala mjukuu wa mtume,
wanataka fun. my opinion, u sound boring....mie mume wangu nilkutana naye
bar, nilikuwa nimepata kinywaji cha kutosha hata gari nikashindwa
kuendesha ikabidi ani-drop home.........been married for 10 years now.....


ha ha haaa, wee mdau ur soo fun loll! ila huyu mwenzetu anahitaji outing
kwa wingi, vinginevyo asubiri mambo ya cinderella
Anonymous  - re:   |2010-08-16 21:45:19
Anonymous wrote:
Pole sana dada yangu!!

Kama ningejua uko wapi au kama unaweza kuweka
contacts zako hapa nitakuwa tayari kuanza mawasiliano nawe.Mimi nina 36
na nahitaji kuoa baada ya kukata shule zangu.Kama uko makini na hili
jambo basi weka contacts zako nikubip.Umenigusa sana na nimeridhia sana
maelezo ya maadili uliyolelewa nayo.Let us take our charge and see
what is in btn us.Look forward to hearing soon from you!!



kama ni mkaka tafwadhali tunaomba uwe serious kwa hili manake sie
wanawake hitimisho letu la mwisho ni ndoa na kuwa na familia bora, so
plse uwe mkweli hope na wewe una maadili mema
Anonymous   |2010-08-16 22:04:29
dada jamani achana na hadithi za cinderella unangojea libahati likundokee, uwe
unatokatoka sio wote wanotoka ni machangudoa, nenda kwenye ma band wanaume wengi
sana waliotulia wanapenda miziki ya band, jumamosi katiza mitaa ya rose
gardern, break point, kapate kinywaji na nyama choma, english premium league
ikianza hapo ndo mwake wanaume wengi wanapenda sana mpira jitahidi uwe unaenda
kuangalia hata kama hupendi tizama mpira kunywa kiwine chako, ikija ofa ya wine
haya ndo mwanzo wa safari na sio lazima ofa ya wine hata mazungumzo ya kawaida
tuu, ila wanaume wengi ili kuanza ukaribu huwa wanatuma kwanza ofa ya kinywaji
unachokunywa na wengine wanatuma contact zao wanampa muhudumu wengine wanaomba
namba alimradi tu apate lao nafasi ya kuzungumza na wewe, uendege na dinner mama
sasa hiyo mambo ya nyumbani kazini mhh inachelewesha bahati, mwenzio nilikuwa
kama wewe, leo na 38 sina mume wala mtoto nilishaliaga nikaomba na kufunga
Anonymous   |2010-08-17 03:35:54
Usitkate tamaa...mungu atakupa tu mume...muhimu badilisha kidogo style ya maisha
yako...jitahidi unapotoka kazini chakula cha jioni nenda ukale kwenye hotel
nzuri nzuri hata kama kwa mwezi mara 2, nenda bar kaagzie nyama choma na soda
unywe (japo mume wa bar si mume kwa mie, sabab sipendi mwanaume mlevi na
anaeshinda bar).....sehemu kama steers na nyinginezo uwe unapita pita kula
chakula cha jioni au hata kunywa juice n.k.....hata usiku kwenda kwenye band
n.k....unaweza kutana na marafiki wapya n.k.......USIKATE TAMAA HAO WALIOOLEWA
NI BAHATI TU WALA SI KWAMBA ATI WANAJUA KU DO au kupika..omba mungu pia.....
Kinyamana   |2010-08-17 04:06:25
Dada uctuongopee kuwa mkweli, kama wewe ni kazini na nyumbani tu hao Wanaume
Wanne ulikuwa unaenda nao wapi?
Anonymous   |2010-08-17 04:13:57
good things come to those who wait
Anonymous   |2010-08-17 08:31:21
alikuwa anakutana nao gheto mwezi mara moja mpaka abembelezwe wenzie dozi
wakatoa daily mpaka ikakolea akaachwa ukipata bwana mpe dozi mara elfu
usikatishe mpaka sumu ijae mwilini hakuachi ukikatiza dozi anakuwa sugu kalagha
bhao
Anonymous   |2010-08-17 04:41:38
Ila pia dada si wote mungu kapanga waolewe inawezekana ukaishi maisha ya raha
zaidi kwa kutokuolewa na ukaolewa na wala usiwe na raha na maisha ya ndoa ila
tayari inakusumbua kwa kutokuolewa ila tunatakiwa kuridhika kwa kila hali
tunayokuwa nayo
Anonymous   |2010-08-17 04:44:43
I will pray for u and u will get a husband, it doesnt matter what is ur
lifestyle coz God said he can do all things beyond our imaginations and our
thinking be urself if u believe in staying at home after work dont change there
is good thing in that and it says u love be a family person remember to talk to
God in all your doing and he shall do more for u, soma yeremia 33:3,
Anonymous   |2010-08-17 16:46:55
God help those who help themselves..Omba dada pia jibidiishe mingle makazini
kwenye events kanisani/msikitini Mungu atakusaidia. Niliomba sana mie pia na
kujibidiisha Mungu akanijalia mume mzuri sana ananitunza vizuri kwakweli life
raha mustarehe
Bigga   |2010-08-17 05:01:42
dada kuolewa siyo kila kitu katika maisha, ishi maisha yako, one day yes,
utapata mwenza wa maisha. usiwe desperate kuolewa, utakurupuka utaolewa
usipopendwa ama usipopenda. be careful
Nancy   |2010-08-17 05:05:45
Kuna mijitu inajua kujishaua ,,Pole dada omba kwa Bidii na mungu atakupa
mme..achana na hao wanakubeza ,wanne ni wachache sana kwa umri wako huo wa 34
..kunawatu mpaka sasa wana list ya wanaume na hawajaolewa nao .
Cha msingi
Piga magoti ,omba Funga kwa imani mungu atakupa mme wa maisha yako
Love u
Sissy
Anonymous   |2010-08-17 05:17:38
Wala usijali mwaya chagua unayempenda kama hujampata ni kwamba umepangiwa uolewe
late, ingawa kwa umri huo unatamani kuolewa lakini usiruhusu kuwa desparate,
wanaosema wana 10yrs kwenye ndoa ni shida na karaha na kuwa watumwa wa mapenzi
bora uwe na 2yrs lakini ni amani, kuliko ungeolewa 24yrs then mpaka leo unatamka
ninaraha nafurahia watoto.....lol
Anonymous   |2010-08-17 05:26:43
usiwafuate wanaokwambia badili maisha yako nenda kawinde kwenye nyumba za
starehe kama bar, hotel wewe badili kwa kumuomba Mungu na kusocialize like
weddings, maulid, kipaimara and other events na hata midahalo then unachukuwa
contacts za members unawasiliana na kuwatumia msg zenye maadili na vichekesho
vya amani automatically mtakuwa mnatembeleana na hapo si vibaya ukionyesha
kumconvince yule ambaye vigezo vyake unaona utaviweza kuishi naye maana ndoa
zote zina matatizo ila mengine ni stress na mengine unaoweza ukayapotezea. Mungu
akubariki, hujachelewa zamani walikuwa wanaolewa wadogo kwa sababu walikuwa
wanazaa watoto zaidi ya watano sasa wewe ukizidisha wanne tutakucheka. May God
bless you
Anonymous   |2010-08-17 06:30:27
"Kuna waanawake wengi mji huu wanatabia mbaya sana ila kila siku unasikia
mmoja wao kaolewa,mimi sijui hata madisco ni mtu wa kwenda kazini
na kurudi nyumbani yani nimelelewa kwa maadili mema.
"
KWA SENTENSI HIYO MDADA UNAONEKAN AKUWA UKO SO JUGDEMENTAL...KUMUKA
KUWA MAADILI MEMA HAYAONDOI KASORO ZAKO KAMA BIONADAMU..BINADAMU WOTE
TUMEUMBWA TIKIWA NA UDHAIFU FULANI SASA WEWE BADALA YA KUANGALIA BORITI
KATIKA JICHO LAKO...NDIO KWANZA UNATOA KIBANZI KATIKA JICHO
LA MWENZAKO...DUH JAMANI....BADILISHA THE WAY YOU PERCEIVE THINGS NA
IMMEDIATELY UTAONA MABADILIKO...INAWEZEKANA HATA HAO WANNE
ULIOKUWA NAO ULIKUWA UNAWAONA KUWA WANA KASORO NYIINGI NDIO MAANA
IKAISHIA ILIVYOISHIA...YAANI BILA NDOA...GOOD LUCK..
Kakako   |2010-08-19 11:47:05
Mdau chukua 5, you've nailed it...
Dada uliyeomba ushauri jaribu kujichunguza
wewe mwenyewe maana unajijua kuliko mtu mwingine akujuavyo, unaweza kuwa na
tabia njema but kauli yako ikawa kikwazo, unaweza kuwa na kazi nzuri but ukawa
anti-social, judgemental, unappreciative, incosiderate au unaweza ukawa sio
smart/sharp (all round) and so forth... Having said that, nafahamu kuwa ni
vizuri kumuomba Mungu but unaweza usione result mapema mpaka utakapoweza
ku-identify the changes u need to implement from within (character) first and
God will do the rest. Mume huwa haji na tag shingoni kwamba huyu ndiye,
therefore badala ya kujiongezea idadi ya wanaume uliokuwa nao, then jaribu
ku-identify what might have been a turn-off that led to your failed
relationships. If for some reasons tht would be a stumble, then try to consult
them (Ex'es) one by one (i'm sure utakuwa unaweza kuwasiliana nao) na jaribu
kudadisi mambo ambayo hawakupe...
Anonymous   |2010-08-17 06:52:52
usijali ma dia!!!!!! Mungu huwa achelewi! ukiona hajakupa mume ujue muda wako
bado. wewe jaribu kufanya maombi na umuulize Mungu mumeo yupo wapi coz wapo
vijana wa kiume wa umri zaid ya wewe wanatafuta wake so omba tu Mungu
ukutanishwe nao
Anonymous   |2010-08-17 07:00:28
God always give thing for those who wait
Anonymous   |2010-08-17 23:12:05
ndo yalel yale mvumilivu hula mbivu, mwisho unakula iliyooza!
Ambele  - Mr   |2010-08-17 08:23:08
Hi,
Am interested with you, km unaweza naomba tuwasiliane kwa e mail hapo
juu.
Cheers
Mdau Arusha   |2010-08-17 10:39:42
Dada wala usijali sali kwa bidii mungu ndie kiongozi wetu wote,hao wanaoponda
achana nao,tena utapata mume mwaka huu huu mwenye hekima ambae anafaa kuwa
mume,relax dear kila kitu kitakuwa sawa.
mdau   |2010-08-17 11:56:59
dada pole kama advice umepata za kutosha nakuombea kwa mola utapata alie mwema
Anonymous   |2010-08-17 12:00:10
HI dada,
Pole kwa mawazo yaliyokutinga. Nakushauri umuombe sana Mungu maana yeye
ndiye aliyetupangia maisha yetu na ana mipango mema sana juu ya waja wake.
Kama
wengi walivyochangia juu ni kuwa you need to socialize. Not necesarily in bars
and night clubs. Nenda out na uwe charming. Tanzanian men cheat all the time
hivyo uwe tayari kushare huyo utayempata na wengine walio desperate zaidi
yako.

BR
Anonymous   |2010-08-18 21:23:46
Jiongelee we mwenyewe Tzee men hawacheat kama ulivyosema.
Sue KG   |2010-08-17 12:35:21
Dada unayo haki ya kuw worried about your life. Nadhani bado hujakumbana na
wadada marafiki zako ambao wameolewa jamani huwa ni mabingwa kujishaua, they
will keep on asking you the following disgusting and rude questions...when are
you getting married? Dont you know your biological clock is ticking so fast? As
if hawajapitia machungu ya kudate as if wao walienda mteremkooooo ndo wakaolewa.
Mimi nakushauri, kaa muombe Mungu kwa dini yoyote uliyonayomwambie atende
miujiza juu yako na utafanikiwa. Mungu ni mwaminifu hamtupi mja wake. Pia kama
wadau walivyosema get out sometimes, you'll meet new people. Nilikuwa kama wewe
but 2 years ago i met this wonderful man and we're getting married in July next
year.
Anonymous   |2010-08-17 12:43:08
Judgemental and Boring!
Antisocial and not Confident!
Desperate and 'HOLY
than thou'
Men can smell all that,hawasogei.Jaribu kubadilika..Work on those
hapo juu,pray and you shd be fine.Dah kuna wanawake wako desperate nchi hii!!
Anonymous   |2010-08-18 13:44:48
Mume nipo hapa sijui tutawasiliana vipi nina miaka 38 maelezo mengine yatafuatia
.... mwezi mtukufu huu sisi wengine tunatafuta mtu wa kutupikia futari
Anonymous   |2010-08-18 17:43:13
ahahahah mbavu zangu jamani!!!
KINYAMANA   |2010-08-19 04:10:55
AKISHAPIKA FUTARI NA MFUNGO UKIISHA, NDIYO MWISHO WA NDOA SIYO? WEWE HUFAI KUWA
MUME.
Anonymous   |2010-08-19 15:44:45
Uwiiiiiiiiiiiiiii we kk wa futari umenivunja mbavuuuuuuu te tte tehhhhhhhhh
uwiii! Wenzio wako sirias ww unaleta utani! Nenda kinondon makaburini utapata
wa futar wapo kibao!
Muache innocent wa watu ebo!
Man   |2010-08-19 17:00:04
I’m a man, Someone told me about ur story nikaamua nikupe ushauri dadangu.
Wewe si “boring,” sisi tunakuita “strict”. Kila shetani na mbuyu wake
na wewe inabidi upate mwanamme “strict”. Usidanganyike kwenda club kama
hadi umri huo mambo ya club huyajui usianze sasa utachanganyikiwa. Kujimwaga
dancing floor hujui na una aibu. Raha ya clud angalau high kgd na wewe huwezi so
utasinzia na kelele zitakusumbua mwishoni utamiss kitanda chako. Bedides,
wanaume wa club inabidi uwe mwangalifu nao. Wengi ni viwembe watakurusha halafu
wakuteme. Kwa hiyo wazo la club achana nalo. Sasa kumpata mwanamme “strict”
kama wewe inabidi uhudhurie harusi sana na ushone sare. Ukiwa kwenye harusi
jipitishe pitishe ili “Mr. Strict”, mtarajiwa wako akuone. Usicheze cheze
mziki hovyo kwenye harusi kwani “Mr. Strict”hizo sio zake, atakuogopa. Vile
vile kanisani au msikitini usiwe mzito kutoa namba yako. Changamkia semina,
Man (contd)  - Sehemu ya mwisho ya maelezo ya Man hapo juu     |2010-08-19 17:10:57
.......Changamkia semina, warsha na kongamano na safari za nje ya kituo chako
cha kazi na huko hook up na bachelors. Ukipata date ifuatilie ipasanyo na
usisite kumtusha “Mr. Strict” kitandani. Ukiwa kitandani onesha maajabu
mpaka “Mr. Strict” apige ukunga. Mwambie ulikua umeweka vyote miaka yote kwa
ajili yake. Kiyandani usiwe “strict”. Kwa sababu “Mr. Strict” naye ana
background kama yako ya kupenda tu kazi, maendeleo, siasa na kusoma magazeti,
atachanganyikiwa na kuanza kuzungumzia ndoa. Basi, mtaoana na kuishi maisha raha
mustarehe na kujaliwa watoto “Strict”.
silver  - mimi pia kama wewe   |2010-10-03 11:45:41
mimi pia niko kama wewe, usijali dada yangu mungu ametupangia huko mbeleni. so
wewe peke yako tupo wengi sana wa miaka kama yako nami pia natafuta mume.
Mapungo  - dada     |2011-03-30 07:35:40
yaani dada ulikuwa nao wanne tu?kwa nini umekuwa mchoyo namna hiyo?miaka yote
hiyo wanne ni wachache.imagine mimi nikiwa form 4 tayari wa 5 niliwapitia ,tena
enzi hizo bila condom.sasa hivi hazina utamu maana kinga tu every angle.anyway
usikate tamaa tafuta hata wagane wasubiri
valentine  - male     |2011-05-06 11:48:10
ngoja niwe tofauti na wengine nimefurahi kwani umekuwa mkweli naomba nitafute
miriam  - Natafuta mume   |2011-07-27 11:15:26
Natafuta mume wa kunnioa umri wangu miaka 30 awe na miaka 30-35
mwana  - natafuta mume   |2011-08-16 04:56:49
Ni msichana wa miaka 27 Naishi morogoro natafuta mume anehitaji kuwa na mke
aliye serious na hili anitafute kwa email sistmwana@hotmail.com

Naomba
anitafute yule aliye serious tu na si kwa matani
mwana  - natafuta mume   |2011-08-16 05:06:56
Natafuta mume kati ya umri wa miaka 30-37 awe muislam
Vanluck  - Honour n prey 2 God!   |2011-09-25 18:41:39
Mungu ndo kila kitu sister,mueleze hili.
Jichunguze mwenendo wako wa life thn
fahamu kasoro zako,mfano-hasira,uvivu,ukosoaji ulozidi,exegrations,n.k. Alafu
control ye self!
Write comment
Name:
Email:
 
Website:
Title:
UBBCode:
[b] [i] [u] [url] [quote] [code] [img] 
 
 
:confused:8):lol::x:P:oops::cry::evil::twisted::roll::wink::!:
:?::idea::arrow::blink::dead::coffee::karate::gossip::hahaha::newpost::love::lips:
:no::nono::rofl::shrug::stop::tape::thumbsup::wail::waves::yahoo::yes:
 
Please input the anti-spam code that you can read in the image.

3.26 Copyright (C) 2008 Compojoom.com / Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."

 
 
Find U turn Blog on facebook