|
UTAMADUNI WA MTANZANIA NI UPI??? |
|
Written by Mange
|
|
Tuesday, 10 August 2010 01:17 |
|

Hello mamii,
Mambo...?mimi ni mdau wa u turn na huwa sikosi kupitia na kuingalia blogu yako angalao mara moja kila siku..kwa ufupi i am very addicted to it...
Kumekuwa na mjadala kwa muda mrefu katika sehemu mbalilmbali kuhusu ni upi hasa utamaduni wa mtanzania/mu-afrika na hasa linapokuja suala la mavazi...kumekuwa na mabishano makali mara tu picha na hasa zetu wanwake nzinapojitokeza katika mavazi ambayo kwa maoni fulani ni ya kizungu mnoo...sasa hapo mi ndio huwa kila siku siachi kujiuliza maswali...hivi tuna khakika kweli na hicho tunachokisema au kukijadili...utamaduni wetu ni upi hasa? kuvaa nguo fupi ni utamaduni wa kitanzania/kiafrika au wa kizungu?
Mange hii ni picha ya ilipigwa wakati wa enzi za ukoloni katika mkoa mmoja Tanganyika ya enzi hizo na hawa katika picha ni wake za machifu wakiwa na mmoja wa wamisionari wakati huo....sasa wadau tuingalie picha hii na tujadili...naamini wadau watatoa mchango wao ili kuweka sawa the perspective kuhusu utamaduni wa mtanzania/muafrika na hasa linapokuja suala la mavazi
Picha kwa hisani ya blog ya swahilitime
Nakutakia kila la heri katika safari yako ya umama. be blessed mamii.
Yours Mama Jo.
P.S TAFADHALI ISIICHAPE ANUANI YANGU YA E-MAIL HEWANI.
|