25April

NAOMBA USHAURI WA KISHERIA.....

Hi everyone,

Nilifunga ndoa na mume wangu miaka 20 iliyopita dini ya kiislam. Mungu ametujalia watoto watatu (mmoja wa kiume na 2 wakike.  Mume wangu ni mwalimu wa sekondari kwa miaka 16 sasa na mie mwalimu wa elimu ya msingi kwa miaka  14.

Mie na mume wangu tulihamia nje ya nchi (UK) miaka 8 iliyopita kikazi tukafanikiwa kuhama na watoto 2 mtoto wa tatu tulimzaa UK.
TATAZO:

Mwaka 2012 January tuliamua kuanza ujenzi wa nyumba ya kuishi TZ, kwa makubaliano kwamba mie na mume wangu tutakuwa wasimamizi wa ujenzi huo (tusitumie ndugu kusimamia, hofu tutatapeliwa).
Tulikuwa na joint bank account kiasi kila mmoja wetu alitumia pesa kwa adabu ili tutimize ndoto zetu za ujenzi na maisha ya baadae.

Mume wangu alikuja TZ kuanza project ya ujenzi, alifanikiwa kumaliza msingi wa nyumba ya vyumba 12. Mara akaniambia amefanikiwa kupata kazi ya afisa utalii Capetown hvyo hataweza kurudi UK kuungana nasi.
Bila kujua mume wangu aliamua kufunga ndoa ya serikali kwa siri na mdogo wangu ambayo ilimsaidia kumtafutia passport mdogo wangu kama mkewe  wakahamia CapeTown ambako mume wangu alipata kazi ya kufundisha shule ya msingi na sio afisa utalii. Alikataa tusimtembelee akidai anaenda nje ya nchi kikazi. Muda wa kiaka 2 akitoa sababu tusimtembelee na tusiende likizo TZ bila yeye kuwepo nasi.
Mwezi wa kumi na mbili niliamua kwenda likizo TZ na watoto, nikamtumia email kumweleza likizo yetu kwani simu alikuwa hapokei  tena.  Nisitaajabu, majibu ya emaili yangu ni TARAKA kuanzia leo wewe si mke wangu tena.  Nimekuachia watoto ni mali yako, nguo nilizo ziacha UK ni zawadi yako ukipata bwana wa kukuoa mpe avae ili usije nisahau kabisa!

NAHITAJI USHAURI KISHERIA:
1.      Kauza kiwanja chenye msigi wa vyumba 12  na viwanja 2 plain (pesa katumia)
2.      Katoa pesa yote  ktk joint a/c ni mara tu aliponitumia taraka, bila kujali kuwa watoto wanahitaji school   fees ambayo iko ktk a/c hiyo na mie pia hela yangu.
3.      Taraka ni ya email
4.      Kamzalisha mdogo wangu watoto mapacha

HITIMISHO:
1.      Nianzie wapi kisheria kudai haki yangu?
2.       Mwanasheria gani  aweza nisaidia?

Kwa sasa niko TZ nataka nipiganie haki yangu na wanangu.


Wanawake wenzangu, ukiona kwa mwenzio kunawaka moto, kwako Zima moshi usije ukawa moto in future!!!

Asanteni.


22April

JUST IN........

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

You can buy the pieces on the website WWW.MYBONGOLICIOUS.COM or

on ETSY

21April

EASTER SUNDAY........

Happy Easter U-TURN FAMILY......

FROM THE LOWREYS.....

 

Kaka Kenzo....

 

Kakake Keanu huyo....

 

Daddy and Kenzo....

 

These 2, I just love them...

 

Family lunch @ Shutters on the beach... Our fav sunday brunch restaurant.....

 

Keanu and mommy.....

 

Na kitindamimba wangu....

 

Full kucheuliwa...hahahahah

 

Mtu anatafuta nyonyo ...hahahahaha

hajui mama keshavalia ye ataka nyonyo tu...lol...

 

Hey U-turners Im 3 weeks old now.....

 

 

 

 

My 2 sons...Love them soooooo bad.......

 

Ulezi wa dada....... Yani hata restaurant ye ataka beba mtoto atembee nae...lol..

 

Busu from dada.... Mapenzi tele...

 

3 weeks  postpartum....

 

Mama Watatu....

 

 

Muke ya Muzungu....

 

 

Kama nilivyowaambia kitumbo kimekwisha ila nimenenepa zaidi ya wakati nna mimba

now navaa size L. Hizi nguo ni size L yani nilipata shock medium ilivyokataa kuingia...lol...

Kwa hiyo nikipungua hizi nguo pia ziko kwa mgao maana staki kuona nguo size L kabatini kwangu...lol

 

 

I love love these Celine sunnies......

 

Kiss Kiss....

 

With my girl...

 

Huyu hapa toto ake mommy......

 

 

Toto langu, uwiiiii, she is mine....lol....

 

 

Hizi pozi mie hoi...loll

 

Mama watatu na wanae....awwwwww

 

Kabla watoa ushauri hawajaanza jamani mtoto baridi,

it was too hot kakawa kana sweat ndo tukatoa babyshow.... UWIII hivi nani anakumbuka neno babysho not sure kama inaandikwa hivyo...hahahaha

Waiting for Valet to bring our car.....

 

 

 

HAPPY EASTER Y'ALL....

20April

BONGOLICIOUS - PHOTO SHOOT.

What a productive day!! Shot part of my new African Print collection.....

The rest of the collection will be out end of May just in time for summer....

OMG, This dress is to die for....

 

Im in love with her hair....

17April

DAH SIKU YA LEO.....UMESHAWAHI KUPITIA KITU KAMA HIKI???

So siku ya leo nimeanza nayo vizuri ila imeishia vibaya....

At around 12pm I went to the grove kununua sunglasses zingine maana zile nilizovaa jana Kenzo alizikalia jana usiku...

Baada ya hapo I thought ngoja niwe mama mzuri nkawapeleke watoto to the park, so i went back home ,nkamwambia dada hana haja ya kusubiri mpaka 6pm leo asepe zake tu, nkawabeba wanangu wote.Wakati tuko njiani tunaenda kwenye park nkaona niwanunulie watoto drinks and snack wanywe tukiwa park, basi nikasimama kwneye petrol station.

Kumbe nimeshuka kwenye gari nimeacha gari kwenye neutral na sio P. ile nimeingia petrol station tu naskia mtu anapiga honi kama kachanganyikiwa nikaangalia nyuma, uwiiii gari yangu ilikuwa inarudi nyuma yenyewe na wanangu wapo strapped in their car seats ndani ya gari,

kumbe msamaria mwema aliona gari lilivyokuwa linarudi nyuma ndo akawa ananipigia honi. Nilidata, acha nitoke mbio, sijawahi kimbia hivyo in my entire life, ila sasa mwili haukunipa support kwa vile sijakimbia wala kufanya zoezi kwa miaka kadhaa basi nikadondoka chini, PUH, kama gunia vile, tena nimeangukia uso kabisa....Ila sikusikia hata maumivu ya kudondoka nikaamka fasta nikaanza tena kukimbiza gari langu, hapo tayari watu wengine waliokuwa petrol station wamepanick, kuna wanaopiga kelele, kuna wanaokimbiza gari na mimi, yani kama movie vile. Alafu sasa gari linarudi nyuma linaelekea kwenye pump za mafuta. Mungu ni mwema ,yani right before the car hit the pump nilifanikiwa kufungua mlango na kuruka ndani ya gari and hit the brakes. actually kwa kiwewe nilichokuwa nacho sikukumbuka hata ipi kwa zile pedal 3 ni break, I think nilikanyaga ya kwanza ikawa sio ya pili ndo nikapatia... Hapo Kenzo na Bhoke wana scream vibaya mnoooo....

Kuna waliopiga simu 911 tayari yani It was chaos....... Ila i have to admit jamani wenzetu nchi hii wanajua kusaidia jamani, yani watu walivyokuwa wnakimbiza gari na mimi utadhani ni watoto wao humo ndani....

mama mmoja akaanza kulia anasema anahisi kama ni wanae ndo walikuwa kwenye gari...

Basi nikaingia kwenye gari nkwaambia wanangu tunanenda nyumbani  coz of what happened , also because nimeumia ,maana nimechubuka goti,mkoni na elbows zote mbili zimechubuka, Kenzo akatiaje "Noooooo, get my drink first", yani na maumivu yote ilibidi nicheke, watoot jamani imagine bado anataka drink yake, nikashuka, nkaingia petrol station huku natetemeka kwenda kumnunulia hiyo drink, maana alianza na kulia anataka his drink, nimeingia petrol station watu wananiuliza ' OMG you are still buying the drinks' nikawaambia My 3 yr old haelewi anataka drink yake, acha waangue kicheko, yani ilibidi kila mtu acheke.....


iM STILL JUMPY, I NEED TO CALM DOWN......

Kuna mliowahi kupitia kitu kama hiki???? what did you do???

Yani kuanzia leo kabla sijashuka kwenye gari ntakuwa naangalia mara kumi kumi kuwa gear ipo on P....